Hujuma mpya za Israel zaua shahidi Wapalestina 70 Rafah, Khan Younis
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i103604-hujuma_mpya_za_israel_zaua_shahidi_wapalestina_70_rafah_khan_younis
Wapalestina wasiopungua 70 wameuawa shahidi katika mashambulizi mapya ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika miji ya Rafah na Khan Younis, kusini mwa eneo la Ukanda wa Gaza, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 17, 2023 10:24 UTC
  • Hujuma mpya za Israel zaua shahidi Wapalestina 70 Rafah, Khan Younis

Wapalestina wasiopungua 70 wameuawa shahidi katika mashambulizi mapya ya utawala wa Kizayuni wa Israel katika miji ya Rafah na Khan Younis, kusini mwa eneo la Ukanda wa Gaza, huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.

Video zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zimeonesha ndege za kivita za utawala haramu wa Israel zikishambulia kambi za wakimbizi za Al-Nuseirat na Al-Bureij kusini mwa Ukanda wa Gaza na kuwaua shahidi makumi ya Wapalestina.

Video hizo zimeonesha familia za wahanga wa jinai hizo mpya za utawala wa Kizayuni zikiwasaka wapendwa wao kwenye vifusi vya majengo yaliyobomolewa na kuharibiwa na mabomu ya utawala wa Kizayuni. 

Wakati wa hujuma hizo za anga za Wazayuni, maelfu ya Wapalestina walikuwa wamekusanyika katika eneo la Rafah katika mpaka wa kusini wa Gaza na Misri, wakiwa na matumaini kuwa wangeliruhusiwa kuvuka kivuko hicho na kuingia Misri.

Wizara ya Afya ya Palestina imetangaza kuwa, idadi ya mashahidi wa Kipalestina katika mashambulizi hayo ya kutisha ya jeshi la utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza tangu Oktoba 7 imeongezeka na kufikia 2,800.

Mashambulizi mapya ya Wazayuni dhidi ya Wapalestina wa Gaza

Aidha takriban Wapalestina 10,000 wamejeruhiwa kutokana na mashambulizi hayo ya kinyama ya adui Mzayuni dhidi ya raia wasio na hatia katika maeneo tofauti ya Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa Ofisi ya Usajili wa Raia ya Palestina, katika siku 8 za kwanza za vita, familia 47 za Wapalestina zenye idadi ya zaidi ya watu 500 ziliuawa.