HAMAS: Jeshi la Israel linaendelea kufanya jinai kwenye hospitali za Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i107854-hamas_jeshi_la_israel_linaendelea_kufanya_jinai_kwenye_hospitali_za_gaza
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema kuwa, wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wanaendelea kufanya jinai katika hospitali na vituo vya matibabu huko Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Jan 31, 2024 23:30 UTC
  • HAMAS: Jeshi la Israel linaendelea kufanya jinai kwenye hospitali za Gaza

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imesema kuwa, wanajeshi makatili wa utawala wa Kizayuni wanaendelea kufanya jinai katika hospitali na vituo vya matibabu huko Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza.

HAMAS imesisitiza katika taarifa yake ya jana Jumatano kwamba, jeshi katili la utawala wa Kizayuni linaendeleza jinai zake za kinyama katika maeneo na vituo vya shirika la Hilali Nyekundu la Palestina na hospitali ya al Amal huko Khan Yunis ikiwa ni pamoja na kuwashambulia vikali kwa risasi watu walioko kwenye vituo hivyo.

Taarifa hiyo ya HAMAS imesema kuwa, vitendo hivyo vya Wazayuni ni jinai za wazi kabisa za kivita na ni muendelezo wa jinai na uhalifu wa kuchupa mipaka unaofanywa na utawala huo dhalimu dhidi ya wananchi wa kawaida huko Gaza. 

Sehemu nyingine ya taarifa hiyo ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palesina HAMAS imesema kuwa, jamii ya kimataifa ina wajibu wa kutekeleza majukumu yake ya kuulazimisha utawala wa Kizayuni ukomeshe jinai zake za kutisha dhidi ya watoto wadogo, wanawake na raia wa kawaida wasio na ulinzi wa Palestina hasa wa Ukanda wa Gaza.

Wapalestina wawakisalia maiti waliozikwa wa taifa hilo kabla ya kuwazika kwenye kaburi la pamoja

Wakati huo huo miili isiyopungua 100 ya Wapalestina imezikwa katika kaburi la pamoja kwenye mji wa kusini wa Rafah, baada ya askari katili wa utawala wa Kizayuni wa Israel kuiiba miili hiyo katika maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa shirika la habari la Wafa, baadhi ya miili hiyo iliyozikwa tena ilikuwa tayari imeoza na maiti wengine hawakuweza kutambulika. Baadhi ya miili hiyo ilikuwa imenyofolewa viungo.

Jeshi katili la utawala haramu wa Israel ambalo lilikuwa limeiiba miili hiyo ya Wapalestina kutoka hospitalini na kwenye makaburi wakati lilipovamia maeneo mbalimbali ya Ukanda wa Gaza, liliitupa miili hiyo kwenye kivuko cha Karem Abu Salem.