Unicef: Ni muhali kuelezea maafa ya Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i109410-unicef_ni_muhali_kuelezea_maafa_ya_gaza
James Elder msemaji wa Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) amesema kuwa hakuna maneno yanayoweza kuelezea maafa yanayowapata watu wa Gaza.
(last modified 2024-03-12T04:18:09+00:00 )
Mar 12, 2024 04:18 UTC
  • Unicef: Ni muhali kuelezea maafa ya Gaza

James Elder msemaji wa Mfuko wa Kuhudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) amesema kuwa hakuna maneno yanayoweza kuelezea maafa yanayowapata watu wa Gaza.

Shirika la habari la Iran (IRNA) limeripoti kuwa, shirka la UNICEF leo asubuhi limetaka kusitisha vita na kuhitimishwa jinamizi la wakazi wa Ukanda wa Gaza. 

Elder amesema: Watoto wa Gaza wanasumbuliwa zaidi na njaa, vita na utapiamlo.

Watoto wa Gaza wanapoteza maisha kwa njaa 

Wakati huo huo Catherine Russel, Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNICEF ameeleza kuwa watoto wengi wa Ukanda wa Gaza wana utapiamlo na kusisitiza kuwa watoto wa Kipalestina wanaoishi Gaza wanakaribia kupoteza maisha.   

Russel ameongeza kuwa, katika kila watoto 6 walio na umri wa chini ya miaka miwili huko Gaza mmoja ana utapiamlo mkali.

Kuhusiana na suala hili, Idara ya Habari ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina jana usiku ilitahadharisha kuwa idadi ya watoto wa Gaza wanaopoteza maisha kutoka na njaa na kukosa chakula inaongezeka kila siku.