UNRWA: Watu wa kaskazini mwa Gaza wanakabiliwa na njaa
Shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada ya Kibinadamu kwa Wapalestina (UNRWA) limetangaza kuwa misaada ya kibinadamu kwa familia za Wapalestina wanaoishi Ukanda wa Gaza haikidhi hata mahitaji yao ya kiwango cha chini kabisa.
Shirika la habari la Palestina la Shihab limeripoti kuwa, idadi kadhaa ya Wapalestina wameuawa shahidi na kujeruhiwa katika shambulio la jeshi la Israel dhidi ya raia wa Kipalestina katika mtaa wa al-Rashid katika mji wa Gaza jana Jumapili, ambao walikuwa wakijaribu kurejea kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.
Idadi kadhaa ya majeruhi wa Kipalestina walihamishiwa katika hospitali ya Al-Awda katika Kambi ya Al-Nuseirat, katikati mwa Ukanda wa Gaza. Wakati huo huo duru za Wapalestina zimearifu kuwa baadhi ya raia wa Kipalestina walikusanyika karibu na mtaa wa Al-Nabulsi wa Mtaa wa Al-Rashid katika mji wa Gaza, wakiwa na matarajio ya kuona familia zao baada ya taarifa za baadhi yao kurejea kutoka kusini kuelekea kaskazini.
Ripoti nyingine zimearifu kuwa, ndege za kivita za utawala wa Kizayuni jana Jumapili zilishambulia maeneo ya magharibi mwa mji wa Khan Yunis, kusini mwa Ukanda wa Gaza na maeneo ya magharibi mwa nchi hiyo.

Taarifa ya Wizara ya Afya ya Palestina imeeleza kuwa wanajeshi wa utawala ghasibu vya Kizayuni wametekeleza jinai 4 katika Ukanda wa Gaza usiku na mchana siku kadhaa zilizopita na kuwaua shahidi Wapalestina 43 na kujeruhi wengine 62.