Bunge la Iraq: Jibu la Iran kwa Israel ni haki halali
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i110654-bunge_la_iraq_jibu_la_iran_kwa_israel_ni_haki_halali
Naibu Spika wa Bunge la Iraq amesema kuwa hatua ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kuurushia makombora na ndege zisizo na rubani (droni) utawala wa Kizayuni ni haki ya kimaumbile na iliyostahiki.
(last modified 2024-04-15T04:31:12+00:00 )
Apr 15, 2024 04:31 UTC
  • Bunge la Iraq: Jibu la Iran kwa Israel ni haki halali

Naibu Spika wa Bunge la Iraq amesema kuwa hatua ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ya kuurushia makombora na ndege zisizo na rubani (droni) utawala wa Kizayuni ni haki ya kimaumbile na iliyostahiki.

Mohsen al Mandalawi Naibu Spika wa Bunge la Iraq ameeleza kuwa, kwa mujibu wa sheria za kimataifa hatua ya Iran ya kujibu shambulio la Israel katika ubalozi mdogo wa nchi hii huko Damascus Syria lilikuwa jibu la kawaida na la halali la Iran.  

Wakati huo huo katika mazungumzo ya simu na Hossein Amir Abdollahian Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran, Faisal al Miqidad Waziri wa Mambo ya Nje wa Syria pia amelaani shambulio la utawala wa Kizayuni katika ubalozi mdogo wa Iran mjini Damascus na kusema: Jibu lililotolewa na Iran kwa hujuma ya Israel ni hatua halali kwa ajili ya kujitetea. 

Faisal al Miqdad 

Al Miqdad pia amelaani mashambulizi ya mara kwa mara ya utawala wa Kizayuni dhidi ya mamlaka ya kujitawala na ardhi ya Syria khususan katika maeneo ya raia kama vile mashambulizi katika viwanja vya ndege vya Damascus na Halab na hujuma dhidi ya miundombinu mingine ya Syria yaliyopelekea kuuliwa na kujeruhiwa raia kadhaa wa Syria.