Hamas: Utawala wa Kizayuni abadan hauwezi kuwapigisha magoti Wapalestina
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imeashiria kuendelea jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina na kusema, Wazayuni kamwe hawawezi kuwapigisha magoti wananchi wa Palestina.
Hamas imeashiria jinai za kikatili za adui Mzayuni zinazotekelezwa kwa himaya na uungaji mkono wa pande zote wa serikali ya Marekani na kusisitzia kuwa adui Mzayuni abadan hatoweza kuwapigisha magoti Wapalestina.
Hamas imesema kuwa kushtadi mashambulizi ya jeshi la utawala wa Israel unaiokalia Quds kwa mabavu na uvamizi wake dhid ya maeneo mbalimbali ya mji wa Gaza ni katika kuendelea mauaji ya kimbari ya kila uchao ya Israel dhidi ya Wapalestina.
Harakati hiyo ya muqawama imeitolea wito jamii ya kimataifa na Umoja wa Mataifa kutekeleza majukumu yao ili kusitishwa jinai za mauaji ya kimbari dhidi ya Wapalestina.
Wakati huo huo kundi la Saraya al Quds ambalo ni tawi la kijeshi la harakati ya Jihadul Islami ya Palestina limeishambulia kwa makombora kamandi kuu ya utawala wa Kizayuni katika korido ya Netzarim.
Huko nyuma Kanali 14 ya Israel iliripoti kwa kuwanukuu maafisa wa jeshi la utawala huo ghasibu kuwa kwa kuzingatia uchunguzi uliofanywa kuhusiana na operesheni ya wanamuqawama wa Palestina ya Kimbunga cha al Aqsa ya tarehe 7 Oktoba mwaka jana, baadhi ya makamanda wa Israel wanaamini kuwa jeshi hilo limefeli katika majukumu yake huko Gaza.