Sayyid Hassan Nasrullah: Israel inapitia siku mbaya zaidi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i113932-sayyid_hassan_nasrullah_israel_inapitia_siku_mbaya_zaidi
Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema katika hotuba yake kuwa Utawala wa Kizayuni unapitia siku mbaya zaidi za historia yake bandia na kuwa mwishowe utawala huo utalazimika kusimamisha vita huko Ukanda wa Gaza.
(last modified 2024-07-11T03:31:30+00:00 )
Jul 11, 2024 03:31 UTC
  • Sayyid Hassan Nasrullah: Israel inapitia siku mbaya zaidi

Katibu Mkuu wa Harakati ya Hizbullah ya Lebanon amesema katika hotuba yake kuwa Utawala wa Kizayuni unapitia siku mbaya zaidi za historia yake bandia na kuwa mwishowe utawala huo utalazimika kusimamisha vita huko Ukanda wa Gaza.

Sayyid Hassan Nasrullah aliashiria jana mwanzoni mwa hotuba yake kuhusu uwepo wa Hizbullah katika harakati ya kuiunga mkono Gaza na kusema: 'Lengo la harakati ya Lebanon ya kuiunga mkono Gaza ni kumchosha adui upande wa kaskazini na kutotoa mwanya wa kutatua vita katika Ukanda wa Gaza kwa maslahi ya adui; na hii leo tunaona kuwa jeshi la Israel halina uwezo wa kuhamia upande wa kaskazini kwa sababu linahofia kujipenyeza makundi ya muqawama hasa baada ya kupoteza vifaa vyake vya ujasusi katika eneo.'

Jeshi la adui 

Sayyid Hassan Nasrullah ameongeza kuwa: 'Malengo ya vita vyetu na utawala wa Kizayuni yanatimizwa kila siku na kusambaratika adui na jeshi lake katika nyanja zote pia kunathibitisha suala hili. Kupitia vita hivyo, tunaweza kumvuruga adui katika hujuma zake dhidi ya Gaza na kumfanya aelewe kwamba mapigano yatasitishwa upande wa kaskazini iwapo uvamizi dhidi ya Gaza utasitishwa.'

Sayyid Hassan Nasrullah ameashiria namna jeshi la utawala wa Israel unaoikalia Quds kwa mabavu unavyokabiliwa na upungufu wa wanajeshi na kusema: 'Adui Mzayuni sasa anapitia siku mbaya zaidi za historia yake.'

Katika hotuba yake ya jana, Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon ameashria pia uchaguzi wa Rais wa Iran na kushukuru ujumbe wa kuunga mkono muqawama wa Rais mteule wa Iran Masoud Pezeshkian. Amesema, msimamo huu unathibitisha misingi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran katika kuunga mkono muqawama.