Kwa mara ya kwanza Hizbullah yakishambulia kituo kikubwa cha jeshi la anga la Israel
Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Lebanon, Hizbullah, kwa mara ya kwanza, imeshambulia kwa makombora kambi kubwa ya jeshi la anga la utawala wa Kizayuni wa Israel, ikiwa ni sehemu ya ulipizaji kisasi dhidi ya ukatili unaofanywa na utawala huo ghasibu.

Ndege hizo zisizo na rubani zimekilenga kituo cha vifaa cha Kitengo cha 146 kilichoko kaskazini mwa kijiji cha Sheikh Dannun, mashariki mwa Nahariya.
Wanamapambano wa Muqawama wa Kiislamu wa Lebanon wameshambulia pia kwa makombora kambi ya Shraga iliyoko kaskazini mwa mji unaokaliwa kwa mabavu wa Akka.
Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimeripoti kuwa walowezi wawili wabeba silaha wameuawa huko Nahariya na wengine kadhaa wamejeruhiwa kutokana na mashambulio hayo.
Operesheni za mashambulizi za Hizbullah ni jibu kwa uvamizi wa utawala ghasibu wa Israel dhidi ya Lebanon, ambao umepelekea Walebanon zaidi ya 3,000 kuuawa shahidi tangu Oktoba 2023.
Harakati hiyo ya Muqawama wa Kiislamu imeshadidisha operesheni zake za kulipiza kisasi dhidi ya utawala wa Kizayuni tangu Katibu Mkuu wa harakati hiyo Sayyid Hassan Nasrullah alipouawa shahidi mwezi Septemba katika shambulio la kinyama lililofanywa na jeshi la Kizayuni.../