Kuendelea jinai za Israel katika Ukanda wa Gaza mbele ya kimya cha wanaodai kutetea haki za binadamu
Umoja wa Mataifa umesema kukwa umekumbwa na wasiwasi mkubwa kuhusu hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Ghaza na kutahadharisha kuwa eneo hilo linapitia katika hali ngumu sana tangu kuanza vita dhidi ya ukanda huo.
Jens Laerke, Msemaji wa Ofisi ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa ameashiria kuwa hadi sasa zimepita siku zaidi ya 50 ambapo hakuna msaada wowote wa kibinadamu uliofika Gaza huku utumaji wa bidhaa za kibiashara pia ukiwa umesimamishwa kwa muda mrefu sasa na kutahadharisha kuwa: Ukada wa Gaza hivi sasa uko katika hali mbaya zaidi tangu kuanza vita na mauaji ya kimbari kutokana na utawala wa Israel kuzuia kuingia misaada ya kibinadamu. Amesisitiza kuwa: Kuna dalili za wazi za kuweko maafa makubwa, na hali ya kibinadamu ni mbaya zaidi huko Gaza kutokana na kuendelea vita na mauaji ya kimbari ya Israel.

Utawala wa Kizayuni tangu tarehe 18 Machi mwaka huu baada ya kukiuka makubaliano ya usitishaji vita, si tu kuwa umefunga njia za kugawa misaada na kuingiza bidhaa za chakula na dawa katika Ukanda wa Gaza lakini pia Israel umefanya mashambulizi makubwa ya anga katika maeneo mbalimbali ya Gaza, ikiwa ni pamoja na kuzishambulia na mahema ya wakazi wa Gaza, jambo ambalo limesababisha kuongezeka kwa idadi ya vifo vya raia wa Kipalestina. Takwimu zinaonyesha kuwa zaidi ya watoto 600 wameuawa shahidi katika mashambulizi haya tajwa.
Aidha mamia ya Wapalestina wanaugua maradhi mbalimbali na hawana chakula. Dakta Marwan al Hams Mkurugenzi wa Hospitali za muda katika Ukanda wa Gaza ameeleza kuwa: Gaza inakabiliwa na vifo vingi vya majeruhi na wagonjwa, na hali hii imetokea kutokana na kuendelea mashambulizi ya Wazayuni na kuzuiwa wagonjwa kuondoka Gaza na kuelekea nje ya ukanda huo kwa ajili ya matibabu.
Hali hii ya kusikitisha inaendelea huku dunia ikitazama tu bila ya kuchukua hatua zozote za maana za kukabiliana na janga hili la kibinadamu. Ripoti zinaonesha kuwa vikwazo na ukwamishaji wa kikatili unaofanywa na Israel wa kuzuia kupelekwa bidhaa za chakula na dawa na huduma nyingine muhimu huko Gaza vimeyafanya maisha ya Wapalestina zaidi ya milioni mbili kuwa jinamizi lisilokwisha.

Ni wazi kuwa baada ya kuvunjika makubaliano ya kusitisha vita kwa lengo la kutoa mashinikizo ya kiwango cha juu kwa harakati ya mapambano ya ukombozi za Palestina kwa kisingizio cha kulinda usalama; utawala wa Kizayuni umeamua kuwaadhibu raia wote wa Gaza kwa kuwasababisha njaa na magonjwa mbalimbali. Richard Falk, Ripota Maalumu wa zamani wa Umoja wa Mataifa kuhusu Palestina amesisitiza kwa kusema: "Kinachotokea Gaza hivi sasa ni adhabu ya pamoja ambayo inakiuka sheria za kimataifa."
Chanzo cha mgogoro huu kinapaswa kuchunguzwa katika kalibu ta sera za uvamizi na ukaliaji mabavu za Israel ambazo kwa miaka mingi sasa utawala wa Kizayuni unakandamiza haki za msingi za Wapalestina. Hivi sasa imepita miaka mingi ambapo Gaza imekuwa jela kubwa kuwahi kushuhudiwa duniani huku wakazi wake wakinyimwa mahitaji ya kimsingi kabisa ya kibinadamu. Mwandishi wa habari wa Israel Gideon Levy ameandika katika gazeti la Haaretz kwamba: "Sera za Israel dhidi ya Gaza si tu ni za kinyama, bali pia zinafedhehesha na dunia inapaswa kukomesha hali hii."
Ni wazi kuwa licha ya mauaji na ukiukwaji wote wa sheria za haki za binadamu unaofanywa na Israel lakini Marekani na waitifaki wake wa Magharibi mbali na kukaa kimya mkabala wa jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni, wamekuwa bega kwa bega na utawala huo katika jinai zake kwa kuutumia silaha na kuunga mkono sera za Israel katika mauaji ya imbari dhidi ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza. Hii ni katika hali ambayo nchi za Magharibi daima zimekuwa zikipiga nara za kuuunga mkono haki za binadamu na kudai kuunga mkono amani duniani. Lakini kinachoshuhudiwa sasa na kushtadi wimbi la jinai za Israel zilizofikia kiwango cha mauaji ya kimbari. Mamia ya watoto wanakabiliwa na hatari ya kifo kwa kukosa dawa za matibabu na chakula. Watoto hao hawana chakula, hakuna dawa zozote za matibabu, wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu hawaruhusiwi kuingia Gaza huku idadi ya wagonjwa ikiendelea kuongezeka. Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu imesisitiza kuhusu suala hili kwamba: Hali ya kibinadamu huko Gaza imefikia hatua mbaya ambayo haitaweza kurekebishwa bila hatua na uingiliaji wa haraka wa jamii ya kimataifa.
Katika mazingira hayo, kuendelea kimya na kutochukua hatua mkabala wa jinai za utawala wa Kizayuni kutasababisha maafa ya kibinadamu na mauaji ya kimbariambayo yatabaki kuwa doa kwenye paji la nyuso za watetezi wa haki za binadamu duniani kuwahi kushuhudiwa katika miongo kadhaa.