Magaidi 150 wa Daesh waangamizwa mashariki mwa Syria
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i12694-magaidi_150_wa_daesh_waangamizwa_mashariki_mwa_syria
Jeshi la Syria limefanikiwa kuangamiza makumi ya wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh katika mkoa wa Deir Ez-Zour, mashariki mwa nchi mapema jana Ijumaa.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Aug 05, 2016 23:18 UTC
  • Magaidi 150 wa Daesh waangamizwa mashariki mwa Syria

Jeshi la Syria limefanikiwa kuangamiza makumi ya wanachama wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh katika mkoa wa Deir Ez-Zour, mashariki mwa nchi mapema jana Ijumaa.

Shirika rasmi la habari la Syria SANA limeripoti kuwa, magaidi 150 wa kundi hilo la wakufurishaji wameuawa walipojaribu kushambulia ngome za jeshi hilo katika mji wa Tal Bruk katika mkoa wa Deir Ez-Zour wenye utajiri wa mafuta.

Askari wa Syria wakikabiliana na Daesh

Wanachama wa Daesh wamekuwa wakifanya juu chini kutaka kuudhibiti mkoa huo ulioko katika mpaka wa Syria na Iraq, kwa kuwa umepakana na ngome nyingi za kundi hilo la kitakfiri.

Haya yanajiri siku moja baada ya ndege za kivita za Russia kuulenga msafara wa magari ya kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh, katika mji wa Atarib uliopo katika viunga vya mkoa wa Aleppo kaskazini mwa Syria. Idadi kubwa ya wanachama wa kundi hilo waliripotiwa kuuawa katika hujuma hiyo.

Wanajeshi wa Syria wakipongezana baada ya kuangamiza idadi kubwa ya madaesh mkoani Aleppo mwezi Julai 2016

Magaidi hao wanaoungwa mkono na nchi kama Marekani na Saudi Arabia wamepata pigo kubwa katika siku za hivi karibuni nchini Syria ambapo sasa  wanakimbia ovyo wakiacha nyuma ngome na maeneo waliyokuwa wakiyashikilia kwa miaka kadhaa.

Hivi karibuni jeshi la Syria lilifanikiwa kusonga mbele katika eneo la Tal Hammad viungani mwa mkoa wa Aleppo na kufanikiwa kuwaangamiza magaidi wasiopungua 450 wa kundi hilo la kigaidi.