Hamas yamtaka Mahmoud Abbas asitishe ukandamizaji
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetaka kusitishwa ukandamizaji unoafanywa na Mamlaka ya Ndani ya Palestina kwa wanachama wa harakati hiyo.
taarifa ya Hamas imesema kuwa matamshi yaliyotolewa na Mahmoud Abbas Rais wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina kuhusu mapatano ya kitaifa yanakinzana na hatua zake katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
Harakati ya Hamas imemtaka Mahmoud Abbas akomeshe ukandamizaji unaofanywa na idara za usalama dhidi ya wanachama, wanaharakati na waungaji mkono wa Hamas kwa lengo la kuifuta harakati hiyo katika mchakato wa uchaguzi wa mabaraza ya miji. Taarifa ya Hamas imeongeza kuwa muqawama unamtaka Abbas achukue hatua kivitendo badala ya kupiga nara.
Askari usalama wa Mamlaka ya Ndani ya Palestina wakishirikiana na utawala wa Kizayuni, wanawatia mbaroni wanamapambano wa Kipalestina wakiwemo wapiganaji wa Hamas katika maeneo mbalimbali ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.