Nov 25, 2016 04:54 UTC
  • Ndege za Marekani zashambulia kambi ya wakimbizi Syria, zaua watu kadhaa

Raia kadhaa wa Syria waliokuwa wakiishi katika kambi ya wakimbizi eneo la Al-Raqqah, wamepoteza maisha yao katika shambulizi lililofanywa na ndege za kijeshi za Marekani dhidi yao.

Taarifa kutoa mkoa wa Al-Raqqah, kaskazini mwa Syria zimesema kuwa, ndege za Marekani zimeilenga kambi hiyo ya wakimbizi na kuua watu 10 na wengine wengi kujeruhiwa.

Ndege ya muungano unaoongozwa na Marekani zinatenda jinai dhidi ya raia Iraq na Syria

Shambulizi hilo limetekelezwa ikiwa zimepita siku tatu baada ya ndege za muungano bandia unaoitwa 'Dhidi ya Ugaidi' unaoongozwa na Marekani, kufanya shambulizi jingine katika jiji cha Swalihiyyah kaskazini mwa mkoa wa  Al-Raqqah ambapo raia wengine 10 wa familia moja waliuawa na wengine sita kujeruhiwa.

Wakimbizi wasio na msaada wa Syria wanaolengwa na ndege za kivita za Marekani 

Inafaa kuashiria kuwa, tangu mwezi Agosti mwaka 2014, Marekani na waitifaki wake wamekuwa wakitekeleza mashambulizi ya anga nchini Syria kwa kisingizio cha kupambana na magaidi wa Daesh (ISIS) bila kibali cha Umoja wa Mataifa wala bila ya ushirikiano wowote na serikali ya Damascus. Hadi sasa muungano huo umeshaua mamia ya raia wa nchi hiyo ya Kiarabu wasio na hatia sambamba na kuharibu makazi yao.

Raia wa Syria wakijaribu kuokoa maisha yao

Kwa mujibu wa duru za habari, muungano huo umekuwa ukitoa himaya kwa wanachama wa magenge ya ukufurishaji kila pale magaidi hao wanapokuwa wameshindwa vitani. Kufuatia hali hiyo, hivi karibuni Donald Trump, rais mteule wa Marekani alinukuliwa akisema kuwa, uingiliaji kijeshi wa Marekani nchini Syria kwa kisingizio cha kupambana na ugaidi, lilikuwa ni kosa kubwa sana.

Tags