Hamas: Himaya ya Marekani kwa Israel ni kuunga mkono ugaidi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i21169-hamas_himaya_ya_marekani_kwa_israel_ni_kuunga_mkono_ugaidi
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza kuwa, himaya na uungaji mkono wa Marekani kwa utawala haramu wa Israel ni uungaji mkono kwa ugaidi.
(last modified 2026-03-03T12:46:59+00:00 )
Dec 10, 2016 23:37 UTC
  • Hamas: Himaya ya Marekani kwa Israel ni kuunga mkono ugaidi

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS imetangaza kuwa, himaya na uungaji mkono wa Marekani kwa utawala haramu wa Israel ni uungaji mkono kwa ugaidi.

Hayo yameelezwa na Fawzi Barhoum, msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina HAMAS ambaye amesisitiza kwamba, himaya na uungaji mkono wa kifedha na kijeshi wa serikali ya Marekani kwa utawala wa Kizayuni wa Israel maana yake ni kuunga mkono dhahir shahir vitendo vya kigaidi.

Kiongozi huyo mwandamizi wa Harakati ya Hamas amesema kuwa, misaada ya kifedha na kijeshi ya Marekani kwa utawala vamizi wa Israel lengo lake ni kuongeza uwezo wa kijeshi na mfumo wa kimakombora wa utawala huo ghasibu hatua ambayo bila shaka ni kujaribu kuficha jinai za utawala huo katili dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina na wananchi wote wa eneo la Mashariki ya Kati.

Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel

Fawzi Barhoum amesema, uungaji mkono wa Marekani kwa utawala ghasibu wa Israel unaotenda jinai kila uchao dhidi ya wananchi wa Palestina maana yake ni kuushajiisha utawala huo uendelee kutenda jinai dhidi ya Wapalestina na hivyo kuzidi kukiuka sheria za kimataifa.

Msemaji huyo wa Hamas amesisitiza kuwa, misaada hiyo ya Marekani imekuwa ikiupa ndisha kiburi utawala dhalimu wa Israel na kuufanya uendelee kuzikalia kimabavu ardhi za Palestina.