PGCC: Hizbullah ni taasisi ya kigaidi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i2332-pgcc_hizbullah_ni_taasisi_ya_kigaidi
Nchi sita wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi zimeiweka Harakati ya Muqawama ya Lebanon Hizbullah ambayo inaendesha mapambano dhidi ya utawala ghasibu wa Kizayuni na magaidi huko Syria katika orodha eti ya magaidi.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Mar 03, 2016 03:10 UTC
  • PGCC: Hizbullah ni taasisi ya kigaidi

Nchi sita wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi zimeiweka Harakati ya Muqawama ya Lebanon Hizbullah ambayo inaendesha mapambano dhidi ya utawala ghasibu wa Kizayuni na magaidi huko Syria katika orodha eti ya magaidi.

Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi jana Jumatano liiliiweka harakati ya Muqawama ya Hizbullah na makundi yote yenye mfungamano na harakati hiyo kwenye orodha eti ya waungaji mkono ugaidi, kwa lengo la kuishinikiza zaidi harakati hiyo ambayo ina nafasi kuu katika matukio ya ndani ya Lebanon na ambayo inaendesha mapambano dhidi ya utawala ghasibu wa Kizayuni na vile vile ikiwa na nafasi muhimu katika kutatua mgogoro wa Syria.

Nchi za kusini mwa Ghuba ya Uajemi mwaka 2013 pia ziliwawekea vikwazo baadhi ya wanachama wa Hizbullah kufuatia kuweko kijeshi Hizbullah katika mgogoro wa Syria. Aidha mwaka huo huo baadhi ya nchi wanachama wa Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi ikiwemo Saudi Arabia, Imarati na Bahrain ziliitaja harakati ya Hizbullah ya Lebanon kuwa ni kundi la kigaidi.