Mar 15, 2017 07:08 UTC
  • Jeshi la Syria lakomboa misikiti mitatu toka mikononi mwa Daesh

Jeshi na vikosi vya kujitolea vya wananchi wa Syria vimekomboa misikiti mitatu iliyokuwa chini ya udhibiti wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh, mashariki mwa mji wa Damascus.

Duru za kijeshi zimeripoti kuwa, misikiti iliyokombolewa na jeshi la Syria ni ile ya al-Noman, al-Hussein na al-Qassem, iliyoko katika eneo la al-Qaboun, mashariki mwa Damascus.

Habari zaidi zinasema kuwa, magenge hayo ya kigaidi yamekuwa yakiitumia misikiti hiyo kupanga njama na harakati zao za kigaidi.

Kikao cha Astana

Wakati huo huo, jeshi la Syria limefanikiwa kutibua shambulizi la kigaidi ambalo Daesh ilikuwa inataka kutekeleza katika mkoa wa mashariki wa Dayr al-Zawr. Mashambulizi ya mabomu yalitokea mjini Damascu Jumamosi ikliyopita na kuua na kujeruhi makumi ya raia wasio na hatia. 

Haya yanajiri katika hali ambayo, duru ya tatu ya mazungumzo ya Astana inatazamiwa kuanza leo Jumatano kwa kuhudhuriwa na wawakilishi wa Iran, Russia na Uturuki pamoja na mwakilishi wa Jordan, Bashar al-Jaafari anayeiwakilisha serikali ya Syria na mwakilishi wa Umoja wa Mataifa.

Duru ya kwanza ya mazungumzo ya amani ya Syria ya Astana ilifanyika tarehe 23 na 24 Januari na ile ya pili ilifanyika tarehe 15 na 16 Februari katika mji mkuu wa Kazakhstan.

Tags