Iran yalaani shambulizi la kigaidi Sinai, yataka dunia kushirikiana zaidi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i31470-iran_yalaani_shambulizi_la_kigaidi_sinai_yataka_dunia_kushirikiana_zaidi
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani shambulizi la kigaidi lililofanyika jana katika eneo la Sinai nchini Misri na kuua makumi ya watu.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Jul 07, 2017 22:21 UTC
  • Iran yalaani shambulizi la kigaidi Sinai, yataka dunia kushirikiana zaidi

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amelaani shambulizi la kigaidi lililofanyika jana katika eneo la Sinai nchini Misri na kuua makumi ya watu.

Bahram Qassemi ametahadharisha kuhusu wimbi jipya la mashambulizi kipofu ya kigaidi yanayofanywa na wanachama wa kundi linaloshindwa na kuangamizwa katika maeneo mbalimbali ya dunia la Daesh na kutangaza mshikamano wa serikali ya Iran na familia za wahanga wa shambulizi hilo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema, kutapakaa na kukimbia ovyo wanachama wa kundi lililoshindwa na kusambaratika la Daesh ambalo limepata kipigo kikali huko Iraq na Syia ni hatari kubwa kwa kanda ya Mashariki ya Kati na maeneo mengine ya dunia. Vilevile ametahadharisha kuhusu siasa za kutumia ugaidi kama wenzo wa kufikia malengo haramu zinazotekelezwa na baadhi ya nchi za Magharibi na kusema mwenendo huo unaweza kusababisha wimbi kubwa na jipya la mashambulizi ya kigaidi katika maeneo mbalimbali ya dunia. 

Polisi ya Misri, Sina

Askari 26 wa jeshi la Misri na magaidi 40 wameuawa baada ya gari lililokuwa limetegwa bomu kulipuka katika kituo cha upekuzi cha jeshi katika Peninsula ya Sinai huko kaskazini mwa nchi hiyo. Wanajeshi wengine 33 wamejeruhiwa katika shambulio hilo. Kundi la kigaidi la ISIS au Daesh limedai kuhusika na hujuma hiyo.