ISIS inatekeleza 'jinai dhidi ya binadamu'
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i3151-isis_inatekeleza_'jinai_dhidi_ya_binadamu'
Wabunge nchini Marekani wamepitisha azimio la kutangaza kundi la kigaidi la Daesh au ISIS kuwa linatekeleza mauaji ya kimbari nchini Iraq na Syria.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 15, 2016 23:28 UTC
  • ISIS inatekeleza 'jinai dhidi ya binadamu'

Wabunge nchini Marekani wamepitisha azimio la kutangaza kundi la kigaidi la Daesh au ISIS kuwa linatekeleza mauaji ya kimbari nchini Iraq na Syria.

Katika azimio lililopitishwa kwa kauli moja Jumatatu, serikali ya Obama imetakiwa kutangaza kuwa jinai zinazotekelezwa na ISIS ni 'jinai za kivita, jinai dhidi ya binadamu na mauaji ya kimbari.

Bunge la Wawkilishi Marekani limeptisha azimio hilo katika hali ambayo magaidi wa ISIS walipata mfunzo yao ya kwanza mwaka 2012 nchini Jordan chini ya usimamizi wa Shirika Kuu la Kijasusi la Marekani CIA kwa lengo la kuiangusha serikali ya Syria. Hivi sasa magaidi hao wanadhibiti baadhi ya maeneo ya Iraq na Syria.

Magaidi hao wamekuwa wakitekeleza vitendo vya kikatili dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Sunni, Shia na pia Wakurdi wa pote la Izadi na Wakristo katika maeneo wanayoyadhibiti.

Marekani na waitifaki wake wamehusika katika uanzishaji makundi ya kigaidi kama vile Al Qaeda na ISIS na kisha kushindwa kidhahiri kuyadhibiti makundi hayo ambayo sasa yanatekeleza jinai za kutisha kote duniani.