Makundi ya Kipalestina yaiunga mkono Harakati ya Hizbullah
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i3304-makundi_ya_kipalestina_yaiunga_mkono_harakati_ya_hizbullah
Makundi kadhaa ya muqawama ya Palestina yametangaza uungaji mkono wao kwa Harakati ya Kiislamu ya nchini Lebanon, Hizbullah
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 18, 2016 04:09 UTC
  • Makundi ya Kipalestina yaiunga mkono Harakati ya Hizbullah

Makundi kadhaa ya muqawama ya Palestina yametangaza uungaji mkono wao kwa Harakati ya Kiislamu ya nchini Lebanon, Hizbullah

Muungano wa makundi ya muqawama wenye makao yake nchini Syria yamefanya kongamano mjini Damascus na kukosoa vikali hatua ya Baraza la Ushirikiano la nchi za Ghuba ya Uajemi na wanachama wa nchi za Kiarabu kwa kudai kuwa Hizbullah ya Lebanon eti ni kundi la kigaidi. Kwa mujibu wa muungano huo, kuitaja harakati ya Hizbullah kuwa ni ya kigaidi ni kuutumikia utawala haramu wa Kizayuni na maadui wote wa Uislamu na Waarabu na kwamba hatua hiyo ya Waarabu ni pigo kwa harakati zote za muqawama zinazopambana na utawala pandikizi wa Israel. Itakumbukwa kuwa hivi karibuni Mawaziri wa Mambo ya Nje wa baadhi ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Kiarabu katika vikao vya mjini Tunis, Tunisia na Cairo, Misri waliitaja harakati ya Hizbullah ya nchini Lebanon kuwa ni ya kigaidi na kuiweka katika orodha ya makundi ya kigaidi suala ambalo limeendelea kukosolewa na kulaaniwa na pande mbalimbali katika nchi za Kiarabu. Kwa mujibu wa weledi wa mambo, hatua hiyo imechukuliwa kwa mashinikizo ya Saudia ambayo inaiona harakati hiyo ya Hizbullah kuwa iliyofelisha njama zake za kutaka kuiondoa madarakani serikali halali ya Rais Bashar al-Assad wa Syria, ni kikwazo kikubwa kwake.