Mwakilishi wa UN ataka kususiwa Israel, Marekani yapinga
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i36009-mwakilishi_wa_un_ataka_kususiwa_israel_marekani_yapinga
Ofisi ya mwakilishi wa Mrekani katika Umoja wa Mataifa imekosoa msimamo wa Ripota Maalumu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Oct 28, 2017 12:09 UTC
  • Mwakilishi wa UN ataka kususiwa Israel, Marekani yapinga

Ofisi ya mwakilishi wa Mrekani katika Umoja wa Mataifa imekosoa msimamo wa Ripota Maalumu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa dhidi ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Taarifa iliyotolewa na mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa imesema Washington ina wasiwasi mkubwa kuhusu matamshi yaliyotolewa na Ripota Maalumu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa aliyetaka kususiwa Israel kiuchumi na katika masuala ya kielimu na vilevile ripoti yake iliyowasilishwa katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa kuhusu kadhia hiyo. 

Ofisi ya balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa imesisitiza kuwa Washington itaendelea kuiunga mkono na kuihami Israel.   

Ripota Maalumu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu za Palestina, Michael Lynk amewaambia waandishi habari katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa kwamba uvamizi wa Israel katika ardhi za Palestina ndio uvamizi wa kijeshi wa muda mrefu zaidi katika dunia ya sasa na hakuna ishara za kukomeshwa uvamizi huo hivi karibuni.

Jeshi al Israel linaendelea kuwanyanya na kuwaua raia wasio na hatia wa Palestina

Michael Lynk ameashiria maazimio ya Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Baraza Kuu la umoja huo yanayotaka kukomeshwa uvamizi wa Israel dhidi ya Palestina na kusema uvamizi wa miaka 50 sasa wa ardhi za Palestina unapaswa kukomeshwa na kwamba Umoja wa Mataifa unapaswa kuomba msaada wa mahakama ya kimataifa kuhusu suala hilo.