Kinara wa kundi la ISIS aangamizwa katika mkoa wa Diyala, Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i38557-kinara_wa_kundi_la_isis_aangamizwa_katika_mkoa_wa_diyala_iraq
Mkuu wa kamati ya usalama ya mkoa wa Diyala, nchini Iraq Bw. Sadiq al-Husseini amesema, jeshi la nchi hiyo limemuua kiongozi muhimu wa kundi la ISIS mkoani Diyala, mashariki mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 05, 2018 11:13 UTC
  • Kinara wa kundi la ISIS aangamizwa katika mkoa wa Diyala, Iraq

Mkuu wa kamati ya usalama ya mkoa wa Diyala, nchini Iraq Bw. Sadiq al-Husseini amesema, jeshi la nchi hiyo limemuua kiongozi muhimu wa kundi la ISIS mkoani Diyala, mashariki mwa nchi hiyo.

Al-Husseini amesema, jeshi hilo limefanya operesheni katika eneo la milimani la Himreen, na kumuua gaidi wa ISIS au Daesh anayeitwa "Abu Ayed".

Idara ya usalama ya serikali ya Iraq imemfuatilia kwa muda mrefu na kugundua kuwa ni kiongozi muhimu wa kundi la ISIS.

Ofisa huyo pia amesema, jeshi hilo limeondoka katika miji na wilaya muhimu za mkoa huo na kukabidhi shughuli za ulinzi wa usalama kwa polisi wa huko.

Mwezi uliopita serikali ya Iraq ilitangaza kutimuliwa magaidi wa ISIS katika maeneo waliyokuwa wameyateka nchini humo. Hata hivyo kuna mabaki ya magaidi hao waliojificha ndani ya wananchi katika maeneo kadhaa ya Iraq.

Waziri Mkuu wa Iraq, Haydar al Abadi

Waziri Mkuu wa Iraq, Haydar al Abadi alitangaza rasmi habari ya kuangamizwa ISIS mwezi uliopita na wakati huo huo kusisitiza kuwa, ushindi mkubwa zaidi ni kulindwa mshikamano na ardhi nzima ya Iraq na kuzuia kugawanyika vipande vipande nchi hiyo. 

Mwaka 2014, kundi la wakufurishaji la Daesh kwa uungaji mkono wa kifedha na kijeshi wa Marekani na waitifaki wake wa Magharibi na Kiarabu ikiwemo Saudi Arabia, liliivamia Iraq na kuteka maeneo mengi ya kaskazini na magharibi mwa nchi hiyo ya Kiarabu na kuanza kufanya jinai za kutisha.