Saudia yapongeza kuwekwa Hizbullah katika orodha ya makundi ya kigaidi
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i51965-saudia_yapongeza_kuwekwa_hizbullah_katika_orodha_ya_makundi_ya_kigaidi
Saudi Arabia imeunga mkono na kupongeza hatua ya hivi karibuni ya Uingereza, ya kuiweka Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon katika jalada lake la makundi ya kigaidi.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Mar 05, 2019 11:07 UTC
  • Saudia yapongeza kuwekwa Hizbullah katika orodha ya makundi ya kigaidi

Saudi Arabia imeunga mkono na kupongeza hatua ya hivi karibuni ya Uingereza, ya kuiweka Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon katika jalada lake la makundi ya kigaidi.

Shirika rasmi la habari la Saudia limenukuu vyanzo vya habari ndani ya Wizara ya Mambo ya Nje ya utawala huo wa kifalme vilivyosema kuwa, Riyadh inaunga mkono kitendo hicho cha Uingereza, na kwamba ni hatua muhimu itakayokuwa na mchango mkubwa katika kupambana na ugaidi.

Kwa mujibu wa duru hizo za habari, Wizara ya Mambo ya Nje ya Saudia imesema hatua hiyo ya kuwekwa Hizbullah katika orodha ya makundi ya kigaidi ya Uingereza inaendana na sera za utawala wa Aal-Saud dhidi ya harakati hiyo ya Muaqawama, kijeshi na kisiasa. 

Mbali na Saudia, Marekani na Israel zimeunga mkono hatua hiyo ya Uingereza dhidi ya Hizbullah

Huko nyuma pia, Saudia imewahi kupongeza vikwazo vya serikali ya Marekani dhidi ya Harakati ya Kiislamu ya Muqawama ya Hizbullah ya Lebanon.

Februari 25, Uingereza ilijiunga na kampeni ya vita vya kila upande vinavyoendeshwa na Israel na Marekani dhidi ya vuguvugu la muqawama unaokabiliana na utawala wa Kizayuni, kwa kupiga marufuku shughuli za harakati ya HIzbullah ya Lebanon nchini humo.