Hizbulllah: Njia pekee ya kuisambaratisha mipango ya Marekani ni muqawanma
Sheikh Ali Damush, mjumbe wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema kuwa, njia pekee ya kusambaratisha mipango ya Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati ni kuendeleza muqawama.
Sheikh Ali Damush ambaye ni Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon ameeleza kwamba, vikwazo vya Marekani na hatua zake za kichochezi dhidi ya muqawama, ni mambo ambayo katu hayawezi kuufanya muqawama ulegeze kamba na kubalisha misimamo yake.
Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, vikosi vya muqawama vitapata ushindi katika vita hivyo na dola la kibeberu la Marekani.
Mjumbe huyo wa ngazi za juu wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesema bayana kwamba, Marekani na madola ya Magharibi yanafanya njama kupitia makundi ya kitakfiri na kigaidi ili kuonyesha Uislamu mbele ya walimwengu kwamba, ni dini isiyo na maadili, ya kikatili na isiyo na utu wala ubinadamu.
Sheikh Ali Damush amesisitiza kuwa, njama zote hizo za Marekani zitafeli na kugonga mwamba na amewataka Waislamu kuamka na kuwa macho na njama za kila leo za Marekani na washirika wao dhidi ya Uislamu na Waislamu.
Naibu Mkuu wa Baraza la Utendaji la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon amesisitiza kuwa, Marekani imekuwa ikitumia mbinu za kikatili zaidi kwa ajili ya kufikia malengo yake katika eneo na kwamba, njia pekee ya kuzishinda njama na mipango hiyo ya Washington ni muqawama, subira na kumtegemea Mwenyezi Mungu.