Salim al Jabouri asisitiza kuundwa serikali yenye nguvu Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i5272-salim_al_jabouri_asisitiza_kuundwa_serikali_yenye_nguvu_iraq
Spika wa bunge la Iraq amesema kuwa nchi hiyo inaweza kuvijua na matatizo iliyonayo iwapo serikali imara itaundwa nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 17, 2016 10:49 UTC
  • Spika wa bunge la Iraq
    Spika wa bunge la Iraq

Spika wa bunge la Iraq amesema kuwa nchi hiyo inaweza kuvijua na matatizo iliyonayo iwapo serikali imara itaundwa nchini humo.

Dakta Salili Abdullah al Jabouri, Spika wa bunge la Iraq amesema leo katika mkutano kuhusu wakimbizi huko Baghdad mji mkuu wa Iraq kuwa nchi hiyo haiwezi kuondokana na matatizo iliyonayo bila ya kuundwa serikali imara nchini humo.

Spika wa bunge la Iraq amesisitiza kuwa chini ya kivuli cha harakati chanya katika siku mbili zilizopita, kikao cha bunge kitafanyika hivi karibuni kwa kuhudhuriwa na wawakilishi wote na kwamba kwenye kikao hicho ambacho Waziri Mkuu atahudhuria pia, kutachunguzwa pendekezo la muundo wa serikali inayotakiwa na kupigiwa kura.

Salim al Jabouri ameongeza kuwa kutekelezwa marekebisho itakuwa moja ya vipaumbele vya utendaji vya bunge la Iraq na bunge hilo litafuatilia mapendekezo yote yaliyowasilishwa na wabunge kuhusu marekebisho.