Sayyid Nasrullah: Saudia ikomeshe mauaji Yemen kwa usalama wake
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i56151-sayyid_nasrullah_saudia_ikomeshe_mauaji_yemen_kwa_usalama_wake
Katibu Mkuu wa Harakati ya muqawama wa Kiislamu ya Lebanon (Hizbullah) amewaasa watawala wa Saudi Arabia wakomesha mashambulizi ya umwagaji damu nchini Yemen kwa maslahi ya taifa lao.
(last modified 2026-03-17T04:36:21+00:00 )
Sep 21, 2019 03:30 UTC
  • Sayyid Nasrullah: Saudia ikomeshe mauaji Yemen kwa usalama wake

Katibu Mkuu wa Harakati ya muqawama wa Kiislamu ya Lebanon (Hizbullah) amewaasa watawala wa Saudi Arabia wakomesha mashambulizi ya umwagaji damu nchini Yemen kwa maslahi ya taifa lao.

Sayyid Hassan Nasrullah aliyasema hayo jana Ijumaa katika hotuba aliyoitoa kwa njia ya televisheni mjini Beirut na kubainisha kuwa, "Saudia inashauriwa isitishe mashambulizi dhidi ya wananchi wa Yemen badala ya kununua mfumo mpya wa ulinzi wa anga."

Amesema mifumo hiyo ya ulinzi haiwezi kuikinga na kuifanya salama Saudia kutokana na mashambulizi ya ndege siziso na rubani za Wayemen.

Moja ya vituo vya mafuta vya Saudia vilivyoshambuliwa na jeshi la Yemen

Hali kadhalika Sayyid Hassan Nasrullah amewataka viongozi wa Riyadh kutafuta muafaka na Iran, akisisitiza kuwa shambulizi lolote dhidi ya Iran haitakuwa kwa maslahi ya Saudia au Imarati.

Siku chache zilizopita, Katibu Mkuu wa Harakati ya muqawama wa Kiislamu ya Lebanon (Hizbullah) alisema vita vyovyote vile dhidi ya Iran vitakuwa na maana ya kuangamizwa na kufutwa katika uso wa dunia, dola pandikizi la Israel.

Kwengineko katika hotuba hiyo, Sayyid Nasrullah ameeleza bayana kuwa, Waziri Mkuu wa utawala haramu wa Israel, Benjamin Netanyahu anaenda mbio ili kuibua taharuki na migogoro katika eneomla Asia Magharibi ili aweze kurejea madarakani, lakini mambo yanaonekana kumuendea segemnege.