Apr 22, 2020 01:37 UTC
  • Unicef: Mamilioni ya watoto Asia magharibi watasumbuliwa na umaskini kwa sababu ya corona

Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (Unicef) umetahadhasriha kuhusu uwezekano wa mamilioni ya watoto katika eneo la Asia magharibi kusumbuliwa na umaskini kutokana na janga la kiuchumi litakalosababishwa na maambukizi ya virusi vya corona.

Shirika la Unicef limetangaza kuwa, katika mwaka huu wa 2020 watoto karibu milioni nane katika eneo la magharibi mwa Asia wataathirika kutokana na kupotea kwa ajira milioni moja na laki saba kulikosababishwa na kufungwa mashirika, kutolipwa mishahara ya wafanyakazi na taathira nyingine za vizuizi vya karantini kwa umma.  

Ted Chaiban Mkurugenzi wa Unicef na katika kanda ya Asia Magharibi na Kaskazini mwa Afrika ameeleza kuwa hivi sasa karibu watoto milioni 110 wamesalia nyumba katika maeneo hayo na hawendi shule kutokana na mlipuko wa maambukizi ya corona. 

Ted Chaiban, Afisa wa Unicef  

Tathmini ya Unicef inaonyesha kuwa, watoto milioni 25 wamekuwa maskini na wakimbizi kutokana na mapigano huko Syria, Yemen, Sudan, katika ardhi za Palestina, Iraq na Libya. Shirika hilo la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa limesema kuwa, linahitaji kiasi cha dola milioni 92 ili kuimarisha mapambano yake dhidi ya taathira mbaya za virusi vya covid-19.

Hadi sasa watu 2,529,094 wameambukizwa virusi vya corona duniani na zaidi ya 174,573 wameaga dunia kwa maambukizi hayo. 

Tags