Wayemen: Muungano vamizi wa Saudia umesimamisha meli 20 zilizobeba chakuka
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i61223-wayemen_muungano_vamizi_wa_saudia_umesimamisha_meli_20_zilizobeba_chakuka
Muungano vamizi wa Saudi Arabi umesimamisha meli 20 zilizobeba chakula na nishati ya mafuta katika bandari ya Jizan.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 26, 2020 03:42 UTC
  • Wayemen: Muungano vamizi wa Saudia umesimamisha meli 20 zilizobeba chakuka

Muungano vamizi wa Saudi Arabi umesimamisha meli 20 zilizobeba chakula na nishati ya mafuta katika bandari ya Jizan.

Kanali ya televisheni ya Al Masirah imewanukuu wasimamizi wa bandari ya Al Hudaydah magharibi mwa Yemen wakisema kuwa, askari wa baharini wa muungano vamizi wa Saudia, wamesimamisha zaidi ya meli 20 zilizobeba zaidi ya tani laki tano za mafuta na chakula kuelekea nchini humo. Kabla ya hapo pia Amin Al Shabati, Msemaji wa Shirika la Mafuta nchini Yemen alinukuliwa akisema kuwa licha ya kuenea kwa virusi vya Corona, muungano vamizi wa Saudia bado unaendeleza uharamia dhidi ya meli zilizobeba nishati za mafuta na chakula baharini.

Raia madhlumu wa Yemen waliozingirwa kila upande

Amesisitiza kwa kusema kuwa Umoja wa Mataiga na muungano huo vamizi wa Saudi Arabia ndio wabeba dhima wa madhara ya yoyote ya kukatika kwa huduma za msingi na za dharura kwa ajili ya watu wa Yemen katika kipindi hiki cha Corona. Wakati huo huo, Shirika la Chakula la Umoja wa Mataifa (WFP) pia limetangaza kwamba jumla ya Wayemen milioni 12 wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula.