Wazayuni wauhujumu Msikiti wa Al Aqsa
(last modified Wed, 10 Jun 2020 04:54:35 GMT )
Jun 10, 2020 04:54 UTC
  • Wazayuni wauhujumu Msikiti wa Al Aqsa

Makumi ya walowezi wa Kizayuni, wakiwa wanapata himaya ya wanajeshi wa utawala wa Israel wameuhujumu Msikiti wa Al Aqsa katika mji wa Quds (Jerusalem).

Kwa mujibu wa taarifa, katika tukio hilo la Jumanne, walowezi hao wa Kizayuni waliuhujumu Msikiti wa Al Aqsa na kuuvunjia heshima huku wakipiga nara dhidi ya Uislamu.

Wiki iliyopit pia makumi ya walowezi wa Kizayuni  waliuhujumu Msikiti wa Al Aqsa na kuwavamia Wapalestina waliokuwa wakiswali.

Kwa mujibu wa duru za Kipalestina, karibu kila siku walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakifanya uvamizi katika msikiti huo lengo likiwa ni kutekeleza njama za kutokomeza utambulisho wa Kiislamu na Kikristo wa Msikiti wa al-Aqsa, kibla cha kwanza cha Waislamu, na badala yake kuweka humo nembo za Kizayuni.

Askari wa Kizayuni wakiuvunjia heshima msikiti wa al-Aqsa

Katika miaka ya hivi karibuni, utawala wa Kizayuni wa Israel umeshadidisha hujuma na uvamizi wake dhidi ya maeneo ya Wapalestina ukifanya njama za kufikia malengo yake haramu katika ardhi za Wapalestina.

Hata hivyo kusimama kidete wananchi wa Palestina hadi sasa kumekwamisha njama na mipango yote ya Wazayuni, zikiwemo njama zake za kubadilisha muundo wa kijamii na kijiografia wa Quds.

Uvamizi huo unakwenda sambamba na ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi katika ardhi ya Palestina.