Mgogoro jeshini Israel, wanajeshi elfu 10 wawekwa karantini
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i65647-mgogoro_jeshini_israel_wanajeshi_elfu_10_wawekwa_karantini
Duru za utawala wa Kizayuni zimetangaza habari ya kuongezeka vibaya maambukizo ya kirusi cha corona ndani ya jeshi la utawala huo dhalimu na kusema kuwa maelfu ya wanajeshi wa Israel wamewekwa kwenye karantini hivi sasa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 08, 2021 03:33 UTC
  • Mgogoro jeshini Israel, wanajeshi elfu 10 wawekwa karantini

Duru za utawala wa Kizayuni zimetangaza habari ya kuongezeka vibaya maambukizo ya kirusi cha corona ndani ya jeshi la utawala huo dhalimu na kusema kuwa maelfu ya wanajeshi wa Israel wamewekwa kwenye karantini hivi sasa.

Mtandao wa Walla News wa utawala wa Kizayuni umetangaza habari hiyo na kuongeza kuwa, idadi ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni waliokumbwa na kirusi cha corona imeongezeka sana kiasi kwamba katika kipindi cha siku mbili tu zilizopita, wanajeshi 167 wa Israel wamepatwa na ugonjwa hatari wa COVID-19.

Mtandao huo umesisitiza kuwa, sehemu kubwa ya wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wako kwenye karantini katika sehemu zao za kazi na kuongeza kuwa, idadi ya wanajeshi wa Israel wanaowekwa kwenye karantini itakuwa kubwa zaidi katika siku zijazo.

Bendera ya utawala wa Kizayuni wa Israel

 

Mtandao huo wa habari wa utawala wa Kizayuni pia umesema, jeshi la Israel hivi sasa limewaweka kwenye karantini wanajeshi wake zaidi ya elfu 10.

Katika upande mwingine, wizara ya afya ya utawala wa Kizayuni imetangaza kuwa, katika kiindi cha masaa 24 yaliyopita, Wazayuni 820 wengine wamegunduliwa kuwa na ugonjwa wa COVID-19 na 26 wamefariki duniani katika ardhi hizo za Wapalestina zilizopachikwa jina bandia la Israel.

Idadi ya Waisrael waliokumbwa na corona tangu mwezi Machi 2020 hadi hivi sasa ni laki nne na 66,377 na waliofariki duniani 3,527 hadi hivi sasa.

Utawala wa Kizayuni umeamua kuweka sheria kali katika ardhi hizo Palestina unazozikalia kwa mabavu kama njia ya kupunguza kasi ya maambukizi ya kirusi cha corona.