Hamas: Mapambano ndiyo njia pekee ya kukabiliana na Israel
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i69492-hamas_mapambano_ndiyo_njia_pekee_ya_kukabiliana_na_israel
Mjumbe wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa kusalimu amri utawala wa Kizayuni wa Israel mbele ya waandamanaji wa Quds inayokaliwa kwa mabavu kumeonyesha kuwa, kusimama kidete na mapambano ndiyo njia pekee ya kukabiliana na utawala huo ghasibu.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 27, 2021 01:41 UTC
  • Hamas: Mapambano ndiyo njia pekee ya kukabiliana na Israel

Mjumbe wa Idara ya Siasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa kusalimu amri utawala wa Kizayuni wa Israel mbele ya waandamanaji wa Quds inayokaliwa kwa mabavu kumeonyesha kuwa, kusimama kidete na mapambano ndiyo njia pekee ya kukabiliana na utawala huo ghasibu.

Khalil al Hayyah amesisitisha udharura wa kufanyika uchaguzi mkuu wa Palestina katika Quds inayokaliwa kwa mabavu na Israel na kusema kuwa, matukio ya karibuni katika eneo hilo takatifu yamethitisha tena kwamba, Wapalestina wanaweza kufanya uchaguzi huko Quds licha ya upinzani wa utawala wa Kizayuni.

Al Hayyah amesema kuwa, wakazi wa Quds wamewaonyesha walimwengu kwamba, hawauogopi utawala wa Kizayuni wa Israel.

Kwa muda wa siku kadhaa sasa, mji wa Baitul Muqaddas unaokaliwa kwa mabavu na baadhi ya miji mingine ya Palestina, inashuhudia mapigano kati ya askari wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel na waandamanaji na waumini Wapalestina wanaolalamikia jinai za utawala huo ghasibu dhidi ya msikiti wa Al Aqsa na Wapalestina.

Jumamosi iliyopita wanajeshi wa Israel walishambulia eneo la Babu al A'mud katikati mwa mji mtukufu wa Quds lakini walikabiliana na mapambano makali ya Wapalestina na hatimaye wakalazimika kurudi nyuma.

Wapalestina wakiingia katika viunga vya Msikiti wa al Aqsa

Baada ya hapo Wpalestina waliondoa vizuizi vya barabarani na kuingia katika viunga vya Msikiti wa al Aqsa. Kitendo hicho kimetambuliwa kuwa ni ushindi ulioibua sherehe na vifijo baina ya Wapalestina.