Haniya: Mapambano ya kukomboa Palestina yamefika nukta muhimu katika historia
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i70236-haniya_mapambano_ya_kukomboa_palestina_yamefika_nukta_muhimu_katika_historia
Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema mapambano ya sasa Ghaza ni nutka ya kihistoria ambayo inathibitisha kuwa mapambano na muqawama ndio njia pekee ya kukomboa ardhi za Palestina na kurejesha haki za taifa hilo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 17, 2021 08:32 UTC
  • Haniya: Mapambano ya kukomboa Palestina yamefika nukta muhimu katika historia

Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) amesema mapambano ya sasa Ghaza ni nutka ya kihistoria ambayo inathibitisha kuwa mapambano na muqawama ndio njia pekee ya kukomboa ardhi za Palestina na kurejesha haki za taifa hilo.

Ismail Haniya Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya HAMAS amezungumza kuhusu hujuma inayoendelea ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Quds (Jerusalem) na msikiti wa Al Aqsa mjini humo na kisha vita dhidi ya Ukanda wa Ghaza na kusema:"Vita ambavyo Ghaza imeingia ni kwa ajili ya kutetea Quds ambayo ni kadhia muhimu zaidi kwa Palestina na Wapalestina."

Haniya amesema kilo kinachojiri katika Ukingo wa Magharibi, Quds na ardhi zilizokaliwa kwa mabavu 1948 kimwaoneysha wote kuhusu utendaji kazi wa kamandi ya kijeshi ya harakati za muqawama.Amesema wote, hasa Wamagharibi ambao kinara wao ni Marekani wanapswa kufahami kuwa kuanzia sasa lazima waamiliane vingine na taifa la Palestina pamoja na makundi ya muqawama.

Kuhusu usitiswahi vita, Haniya amesema amewasisitizia wale wanaofuatilia kadhia hiyo kuwa adui ambayo alianzisha vita afahamu kuwa sukluhu yoyote ambayo haiiendeani na kiwango cha kujitolea taifa la Palestina haikubaliki. 

Utawala ghasibu wa Israel ulianzisha uvamizi dhidi ya Ghaza baada ya Wapalestina katika eneo hii kuandamana kulalamikia vikali ukandamizaji wa Israel dhidi ya Wapalestina katika mji wa Quds (Jerusalem). Kitendo cha askari katili wa Israel kuuvamia Msikiti wa Al Aqsa mjini Quds na kuwahujumu Wapalestina waliokuwa wakiswali katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhani kimehesabiwa kuwa ni kuvuka mstari mwekundu wa Wapalestina na Waislamu duniani.

utawala haramu wa Israel unalenga maeneo ya raia Ghaza

Katika kujibu jinai hizo za Israel makundi ya kupigania ukombozi wa Palestina katika Ukanda wa Ghaza yamevurumisha mamia ya makombora katika miji ya Israel ukiwemo mji wa Tel Aviv na kusababisha hasara kubwa. 

Hadi sasa Wapalestina karibu 218, wakiwemo watoto 58, wameuawa shahidi katika  hujuma hii mpya ya utawala dhalimu wa Israel dhidi ya Ghaza huku wengine zaidi ya 1,235 wamejurhiwa.