Oman yazitaka pande zenye mvutano wa kidiplomasia na Beirut kustahimiliana
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i76374-oman_yazitaka_pande_zenye_mvutano_wa_kidiplomasia_na_beirut_kustahimiliana
Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman imeeleza kusikitishwa na mvutano wa kidiplomasia uliopo kati ya Riyadh na baadhi ya nchi za Kiarabu na Beirut na kuzitaka pande zote kustahamiliana.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 31, 2021 04:33 UTC
  • Oman yazitaka pande zenye mvutano wa kidiplomasia na Beirut kustahimiliana

Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman imeeleza kusikitishwa na mvutano wa kidiplomasia uliopo kati ya Riyadh na baadhi ya nchi za Kiarabu na Beirut na kuzitaka pande zote kustahamiliana.

Taarifa hiyo ya Wizara ya Mambo ya Nje ya Oman imetolewa baada ya ile ya Qatar kufuatia mivutano ulioibuka katika uhusuano wa Saudi Arabia na Lebanon. Taarifa hiyo imeeleza kuwa: Mascut inasikitishwa na kuvurugika uhusiano kati ya nchi kadhaa za Kiarabu na Lebanon na inazitaka pande zote kufikia maelewano. 

Ijumaa usiku Saudi Arabia ilimwita nyumbani balozi wake mjini Beirut kwa kisingizio kuwa Waziri wa Habari wa Lebanon alitoa matamshi ya kuwatetea wananchi wa Yemen mkabala na mashambulizi ya muungano vamizi unaoongozwa na Saudi Arabia; na kisha ikampatia balozi wa Lebanon mjini Riyadh muda wa saa 48 aondoke nchini humo.  

Bahrain pia imefuata kibubusa hatua ya Saudia na kuamua kumfukuza balozi wa Lebanon mjini Manana. Imempatia saa 48 kuondoka nchini humo. 

Wizara ya Mambo ya Nje ya Imarati pia imwita nyumbani balozi wake mjini Beirut na Kuwait nayo imechukua hatua sawa na hiyo kwa kuwarejesha nyumba wanadiplomasia wake waliokuwepo Beirut na kumpatia muda wa saaa 48 afisa kuu wa ubalozi wa Lebanon aondoke Kuwait.  

Kisingizio cha Saudia cha kuibua mivutano katika uhusiano wake na Lebanon ni wkamba, George Qordahi Waziri wa Habari wa Lebanon ambaye kabla ya kuingia katika serikali ya Najib Miqati alikuwa mwendesha vipindi, mwanaharakati wa masuala ya habari na mwandishi mashuhuri wa Lebanon, alisisitiza wazi kuwa kuna udharura wa kusitishwa mashambulizi ya nchi hiyo huko Yemen. Alitamka hayo katika kipindi cha televisheni maarufu kwa jina la " Bunge la Wananchi."

George Qordahi, Waziri wa Habari wa Lebanon