Wanazuoni wa Ahlusunna: Watawala wa Saudia wanaeneza ufisadi wa kimaadili
Wanazuoni wa Ahlusunna kutoka nchi mbalimbali za Kiislamu wametoa taarifa ya pamoja wakipinga ufisadi wa kimaadili na harakati za uharibifu na dhidi ya dini zinazofanywa na utawala wa Saudi Arabia katika ardhi wa wahyi ya Hijaz.
Maulama wa Kisuni katika nchi kadhaa za Kiislamu ambao ni wamachama wa Jumuiya ya Maulama walitoa taarifa jana Ijumaa wakitangaza kuwa, watawala wa Saudia wanaeneza ufuska, utovu wa maadili na vitendo vinavyokinzana na dini kwa makusudi na kwa mpangilio maalumu na wanawatumbukiza vijana kwenye ufuska na kufanya jitihada za kuangamiza jamii ya Saudi Arabia.
Taarifa hiyo imesema: Hatua ya serikali ya Saudi Arabia ya kuzifuata kibubusa nchi za Magharibi inapingana kikamilifu na dini ya Uislamu, tmaadiili na ada za jamii za Waislamu.
Taarifa ya maulama wa Kiislamu imesema kuwa, wanaobeba lawama za hatua hizo katika daraja ya kwanza ni watawala wa Saudia na kisha watu wanaoshiriki katika harakati na shughuli hizo zinazopingana na Uislamu.
Taarifa hiyo imewataka watawala wa Saudi Arabia kukomesha harakakati za makusudi za kuharibu maadili ya Kiislamu, Vilevile imewataka Waislamu na wakazi wa Saudia kwenyewe kutumia njia zote halali kwa ajili ya kupambana na hujuma hiyo yenye uharibifu.
Taarifa hiyo kali ya maulama wa Kiislamu wa nchi mbalimbali imetolewa baada ya Taasisi ya Anasa iliyoanzishwa wmakak 2016 na serikali ya Riyadh kuandaa hafla za ufuka na utovu wa maadili katika ardhi tukufu ya Hijaz. Hafla na shughuli hizo za ufuska na zinazopingana na dini ya Uislamu zimekuwa zikifanyika nchini Saudi Arabia hata baada ya kusimamishwa ibada ya Hija kwa kisingizio cha maambukizi ya virusi vya corona.