Harakati ya Hizbullah ya Lebanon: Tunataka kudumishwa usalama Iraq
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i76662-harakati_ya_hizbullah_ya_lebanon_tunataka_kudumishwa_usalama_iraq
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imelaani kushambuliwa makazi ya Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al Kadhimi. Shambulio hilo lilikusudiwa kumuuwa Waziri Mkuu wa Iraq.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Nov 07, 2021 23:52 UTC
  • Harakati ya Hizbullah ya Lebanon: Tunataka kudumishwa usalama Iraq

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon imelaani kushambuliwa makazi ya Waziri Mkuu wa Iraq Mustafa al Kadhimi. Shambulio hilo lilikusudiwa kumuuwa Waziri Mkuu wa Iraq.

Hizbullah jana ilitoa taarifa na kutaka kufungwa mianya yote kwa wale wote wenye lengo la kuipinduia Iraq kutokea ndani katika kuhudumia njama za maadui. Harakati ya Hizbullah ya Lebanon aidha imetaka kufanyika uchunguzi kamili na wa kina ili kufahamu namna hujuma hiyo ilivyotekelezwa na wahusika wake.  

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon Hezbollah imeongeza inataka inataka kutumiwa busara ili kuzipatia ufumbuzi hitilafu za kisiasa, sambamba na kufanyika mazungumzo, kuwepo subira  na azma ya kutafuta suluhu kwa njia za amani. 

Serikali ya Iraq jana asubuhi ilitangaza kuwa makazi ya Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mustafa Kadhimi yameshambuliwa na ndege tatu zisizo na rubani zilizosheheni mada za milipuko lakini al Kadhimi amenusurika katika hujuma hiyo.  

Akizungumza baada ya jaribio hilo la kutaka kumuua, Mustafa al-Kadhimi alisema: "Niko vizuri namshukuru Mungu na ninatoa wito wa kudumishwa amani na uvumilivu kwa kila mtu kwa ajili ya maslahi ya Iraq."

Waziri Mkuu wa Iraq, Mustafa al Kadhimi