Yemen: Tutashambulia vituo vya mafuta vya Saudia ikiendelea kuiba mafuta yetu
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i84770-yemen_tutashambulia_vituo_vya_mafuta_vya_saudia_ikiendelea_kuiba_mafuta_yetu
Ofisa wa ngazi ya juu wa Yemen ameonya kuwa, vikosi vya jeshi la Yemen vitashambulia vituo vya mafuta ndani kabisa ya Saudi Arabia, iwapo muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Riyadh utaendelea kupora mafuta wa Wayemen.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 15, 2022 07:18 UTC
  • Yemen: Tutashambulia vituo vya mafuta vya Saudia ikiendelea kuiba mafuta yetu

Ofisa wa ngazi ya juu wa Yemen ameonya kuwa, vikosi vya jeshi la Yemen vitashambulia vituo vya mafuta ndani kabisa ya Saudi Arabia, iwapo muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Riyadh utaendelea kupora mafuta wa Wayemen.

Mohammad Tahir Anam, mshauri wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen amesema vikosi vya Yemen havitakaa kimya na kuruhusu Saudia na Umoja wa Falme za Kiarabu ziendelee kukiuka usitishaji vita wa Umoja wa Mataifa na kupora mafuta na gesi ya taifa hilo maskini la Kiarabu.

Anam ameashiria ongezeko la wizi wa mafuta unaofanywa na Riyadh katika mkoa wa Shabwah, kusini mwa Yemen na kusisitiza kuwa, "tutalenga meli za mafuta na gesi za Saudia, pamoja na viwanda vyao vya kusafisha mafuta."

Wakati huohuo, Mohammed Muftah, mshauri mwingine wa Baraza Kuu la Kisiasa la Yemen ametahadharisha kuwa, vikosi vya Yemen vitashambulia meli za Saudia zinazoiba mafuta na gesi asilimia ya Wayemen.

Ansarullah ya Yemen mara kadhaa imeshambulia mashirika ya mafuta ya Saudia

Kwa mujibu wa Ahmad Daris, Waziri wa Mafuta wa Yemen, muungano vamizi wa kijeshi unaoongozwa na Saudi Arabia pamoja na mamluki wao wamepora akiba kubwa ya mafuta ya nchi hiyo.

Licha ya wananchi wa Yemen kuwa na shida kubwa ya chakula na fueli, muungano vamizi wa Saudia si tu umepora mamilioni ya mapipa ya mafuta ya nchi hiyo, lakini umeshadidisha pia hali mbaya ya uhaba wa bidhaa za fueli ilionao Yemen kutokana na kukwamisha na kuzizuia meli za mafuta zinazoelekea nchini humo.