Sheikh Kubais: Netanyahu ndio anayewasimamia Daesh
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i9076-sheikh_kubais_netanyahu_ndio_anayewasimamia_daesh
Mmoja wa Mamufti watajika wa Kisuni mwa Iraq amesema kuwa kundi la kigaidi la Daesh linadhibitiwa na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jun 12, 2016 22:14 UTC
  • Sheikh Kubais: Netanyahu ndio anayewasimamia Daesh

Mmoja wa Mamufti watajika wa Kisuni mwa Iraq amesema kuwa kundi la kigaidi la Daesh linadhibitiwa na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni wa Israel.

Sheikh Ahmad Kubais mmoja wa mamufti mashuhuri wa Kisuni mwa Iraq amesema kuwa kuendesha mapambano dhidi ya kundi la kigaidi la Daesh ni jukumu la Waislamu wote na kwamba kundi hilo la kitakfiri ni miongoni mwa rasilimali za Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala wa Israel.

Mufti huyo wa Iraq amesema kuwa kutopambana na kundi la kigaidi la Daesh kwa wale wote wenye uwezo ni dhambi na kwamba Netanyahu anatoa maagizo kwa viongozi wa Marekani, watawala wa Ulaya na wa baadhi ya nchi nyingine na wao wanatekeleza matwaka ya Israel. Sheikh Ahmad al Kubais amesema kuwa wanachama wa kundi la kitakfiri la Daesh ni mafisadi katika ardhi kwa vitendo vyao vya kuwauuwa kwa umati wanawake na watoto wasio na hatia.