-
Haja ya kuchukuliwa hatua dhidi ya mpango wa Netanyahu wa kuifanya Lebanon kuwa Gaza nyingine
Sep 24, 2024 22:47Katika siku za hivi karibuni, utawala wa Kizayuni umepanua wigo wa jinai zake kutoka Gaza hadi Lebanon na kwa kutumia vibaya uzembe wa taasizi za kieneo na kimataifa, unatekeleza siasa zake katili za kuangamiza kila kitu katika nchi hiyo ya Kiarabu.
-
Sambamba na Lebanon, jeshi la Israel linaendelea kuteketeza roho za Wapalestina wa Ghaza
Sep 24, 2024 07:43Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel linaendeleza mashambulizi na mauaji ya Wapalestina wa Ukanda wa Ghaza mbali na vita vingine vya kinyama lilivyoanzisha dhidi ya Lebanon, ambako hadi sasa limeshaua watu wapatao 500, 100 miongoni mwao wakiwa ni wanawake na watoto.
-
Ayatullah Sistani: Ichukuliwe hatua haraka kukomesha uchokozi wa Israel dhidi ya Lebanon
Sep 24, 2024 07:41Kiongozi wa juu wa kidini na Marjaa-Taqlidi wa Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Iraq Ayatullah Ali al-Sistani ameelezea mshikamano wake na Lebanon wakati nchi hiyo ya Kiarabu na Kiislamu inaendelea kuandamwa na mashambulio ya kinyama ya jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel na ametaka zifanyike juhudi za dharura kusitisha uchokozi huo wa kikatili wa utawala huo na kuwalinda raia wa Lebanon.
-
Utawala wa Kizayuni waendeleza jinai nchini Lebanon, Hizbullah yajibu jinai hizo
Sep 24, 2024 04:00Utawala wa Kizayuni unaendelea kufanya jinai za kushambulia maeneo ya raia nchini Lebanon. Harakati ya Hizbullah nayo imeendelea kujibu jinai hizo kiasi kwamba shughuli za mji wa Haifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu, zimekwamishwa na mashambuizi ya makombora ya Hizbullah.
-
Mkuu wa zamani wa CIA: Hujuma ya kielektroniki ya Israel dhidi ya Lebanon ni 'aina ya ugaidi'
Sep 23, 2024 22:48Waziri wa zamani wa ulinzi wa Marekani ambaye pia aliwahi kuwa mkurugenzi wa shirika la kijasusi la CIA amekiri kwamba shambulio la kielektroniki la utawala haramu wa Israel nchini Lebanon lililohusisha mlipuko wa vifaa vya mawasiliano vya pager ni "aina ya ugaidi."
-
Kuchukua wigo mpana operesheni za muqawama za kukabiliana na vitendo vya kigaidi vya Wazayuni
Sep 23, 2024 22:47Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon na vikosi vya muuqawama wa Kiislamu nchini Iraq vimetekeleza operesheni kadhaa tofauti vikilenga shabaha mbalimbali za kijeshi na kiusalama katika maeneo mbalimbali yanayokaliwa kwa mabavu ambayo yamepewa jina bandia la Israel.
-
Nabih Berri atahadharisha kuhusu hulka ya kupenda vita ya utawala wa Kizayuni katika eneo
Sep 23, 2024 08:32Spika wa bunge la Lebanon ameashiria kuendelea mashambulizi ya utawala wa Kizayuni nchini humo na kusema, Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa utawala huo anafanya kila awezalo ili kuitumbukiza Lebanon na eneo hili katika vita vikubwa.
-
Jibu la awali la Hizbullah kwa chokochoko na uafriti wa Netanyahu
Sep 23, 2024 04:40Baada ya utawala wa Kizayuni wa Israel na kiongozi mwenyewe wa utawala huo bandia Netanyahu kukataa kusitisha vita katika Ukanda wa Ghaza na badala yake kuanzisha mauaji ya kigaidi kupitia hujuma za kimtandao nchini Lebanon, hatua hiyo sio tu imekwamisha juhudi za kurejeshwa amani katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu na eneo kwa jumla,
-
Sheikh Naeem Qasim: Marekani ni mshirika wa jinai za utawala wa Kizayuni
Sep 23, 2024 03:39Naibu Katibu Mkuu wa Hizbullah ya Lebanon amesema Marekani ni mshirika wa mauaji ya kimbari yanayofanywa na utawala wa Kizayuni huko Ukanda wa Gaza na Lebanon.
-
Hizbullah yatwanga Haifa kwa kombora jipya la Fadi, wazayuni wengi waangamizwa
Sep 22, 2024 23:55Harakati ya Hizbullah ya Lebanon imetangaza kuwa imeshambulia kwa makombora kadhaa ya Fadi-1, Fadi-2 na maroketi ya Katyusha viwanda vya kijeshi vya Kampuni ya Rafael, ambayo inajishughulisha na vifaa vya kielektroniki, kaskazini mwa mji wa Haifa huko Israel.