-
UNRWA: Idadi ya Wapalestina waliolazimika kuihama Rafah imefikia 800,000
May 19, 2024 07:14Kwa mara nyingine tena karibu nusu ya Wapalestina wote waliokuwa Rafah, yaani watu wapatao laki nane hivi sasa wapo njiani wakilikimbia eneo hilo ambalo lilianza kushambuliwa na jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel Mei 6 baada ya kutolewa amri na jeshi hilo kuwataka watu wote waondoke katika eneo hilo.
-
HAMAS: Netanyahu anapendelea maslahi yake binafsi kuliko maisha ya wanajeshi wa Israel
May 19, 2024 04:28Tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) limesema kuwa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu wa utawala wa Israel anapendelea zaidi maslahi yake binafsi kuliko maisha ya wanajeshi wa utawala huo ghasibu.
-
OCHA: Kwa kuzuiwa uingizaji misaada, hakuna kilichobaki kugawa katika Ukanda wa Ghaza
May 18, 2024 23:18Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Uratibu wa Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imeonya dhidi ya kuzuiwa uingizaji misaada ya kibinadamu katika Ukanda wa Ghaza na kutangaza kuwa hakuna kilichosalia kwa ajili ya kuwagaia Wapalestina wa eneo hilo.
-
Aliyekuwa Naibu Mkuu wa MOSSAD: Vita vya Ghaza 'havina maana', Israel inaporomoka kiuchumi
May 18, 2024 23:17Naibu Mkuu wa zamani wa shirika la ujasusi la utawala wa Kizayuni wa Israel, MOSSAD Ram Ben-Barak amesema vita vinavyoendelea Ukanda wa Ghaza 'havina maana' na kusisitiza kwamba utawala huo ndio unaopata hasara na unakabiliwa na mporomoko wa kiuchumi.
-
Wapalestina: Tuko tayari kwa 'vita vya muda mrefu' Rafah
May 18, 2024 09:13Tawi la kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) limetangaza kuwa Wapalestina wako tayari kwa vita vya muda mrefu, na kuahidi kukabiliana na uvamizi wa nchi kavu wa Israel dhidi ya Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza na kwingineko.
-
Misikiti zaidi ya 600 yabomolewa Ukanda wa Gaza kufuatia mashambulizi ya Wazayuni
May 18, 2024 03:54Wizara ya Wakfu ya Gaza imetangaza kuwa misikiti 604 imebomolewa kikamilifu katika UKanda wa Gaza kufuatia vita na mashambulizi ya kikatili ya utawala wa Kizayuni.
-
Sami Abu Zuhri: Marekani ni mshirika wa jinai dhidi ya taifa la Palestina
May 18, 2024 00:31Sami Abu Zuhri, Kiiongozii wa Idara ya Kisiasa ya Harakati ya Mapambano ya Kiiislamu ya Palestina HAMAS nje ya nchi amesema kuwa, serikali ya Marekani ni mshirika wa vita dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina.
-
Hamas: Asilimia 70 ya mateka wa Kizayuni wameuawa katika mashambulizi ya Israel
May 18, 2024 00:30Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imetangaza kuwa mashambulizi ya utawala haramu wa Israel katika Ukanda wa Gaza, ambao unakabiliwa na vita vya mauaji ya kimbari ya utawala huo, yameuwa asilimia 70 ya mateka wa Kizayuni, ambao walikuwa wakishikiliwa na harakati hiyo ya muqawama tangu baada ya operesheni ya Kimbunga cha Al Aqsa mwezi Oktoba mwaka jana.
-
Kuenea vuguvugu la wanafunzi dhidi ya Israel kutoka Chuo Kikuu cha Columbia hadi Oxford
May 18, 2024 00:28Wanachama wa jopo la elimu na wafanyakazi zaidi ya 500 wa Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza wameandika barua ya kuunga mkono kambi ya mshikamano na matakwa ya wanafunzi wanaoandamana katika chuo kikuu hicho kuunga mkono Palestina na kulaani jinai zinazofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wa Gaza.
-
Idara ya Habari ya Gaza: Israel imeua zaidi ya maprofesa na wanasayansi 100
May 17, 2024 11:49Idara ya Vyombo vya Habari ya Serikali ya Gaza imetangaza kwamba jeshi la Israel limeua zaidi ya wanasayansi, wasomi, maprofesa wa vyuo vikuu na watafiti zaidi ya mia moja katika vita vinavyoendelea kwenye Ukanda wa Gaza kwa mwezi wa nane mfululizo.