-
Israel kuruhusu Wapalestina waliopindukia miaka 70 tu kuingia Msikiti wa Al Aqsa wakati wa Ramadhani
Feb 19, 2024 07:38Utawala wa Kizayuni wa Israel umeidhinisha mpango wa kuwawekea vizuizi vikali Wapalestina wanaoishi kwenye ardhi zilizoanza kukaliwa kwa mabavu mwaka 1948 na wa mji wa Baitul Muqaddas (Jeruselem) vya kuingia kwenye Msikiti wa Al Aqsa wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, utakaoanza wiki ya pili ya mwezi ujao wa Machi.
-
Yemen: Tumeitwanga meli ya Uingereza na kuitungua ndege isiyo na rubani ya Marekani
Feb 19, 2024 07:36Msemaji wa vikosi vya ulinzi vya Yemen ametangaza kuwa, katika kuonyesha mshikamano na uungaji mkono kwa taifa la Palestina na kujibu mashambulio na uchokozi wa Marekani na Uingereza dhidi ya ardhi ya Yemen, vikosi vya nchi hiyo vimeipiga makombora kadhaa meli ya Uingereza katika operesheni maalumu viliyotekeleza katika Ghuba ya Aden.
-
Anadolu yataja orodha ya silaha zilizofanyiwa majaribio na Israel katika vita vya Gaza
Feb 18, 2024 23:37Shirika la habari la Anadolu la Uturuki limeripoti kuwa utawala wa Kizayuni wa Israel ambao unakabiliwa na kesi ya mashtaka ya mauaji ya halaiki katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ huko Hague Uholanzi umezifanyia majaribio silaha nyingi kwa mara ya kwanza katika mashambulizi yake ya kikatili dhidi ya Gaza tangu Oktoba 7 mwaka jana.
-
Balozi wa Yemen mjini Tehran: Tutapiga shabaha yoyote ya Marekani, Uingereza
Feb 18, 2024 22:57Balozi wa Yemen nchini Iran anasema kuwa vikosi vya jeshi la nchi yake vitashambulia vituo vyote vya Marekani na Uingereza "vinavyoweza kulengwa shabaha" kujibu mashambulizi ya hivi karibuni ya nchi hizo katika ardhi ya Yemen.
-
Afisa wa Mossad: Kila mtu mwenye umri wa zaidi ya miaka 4 wa Gaza ‘anastahili’ kufa kwa njaa
Feb 18, 2024 22:57Afisa wa zamani wa shirika la ujasusi la Israel, Mossad, Rami Igra, amesema Wapalestina wote wa Gaza walio na umri wa zaidi ya miaka 4 wanastahili kukabiliana na sera ya adhabu jumuishi ya Israel ya kunyimwa chakula na misaada ya kibinadamu.
-
Vitisho vipya vya wakosoaji wa Natenyahu; Kuvunjwa Baraza la Mawaziri la Vita
Feb 18, 2024 06:02Sambamba na Waziri Mkuu wa utawala wa Kizayuni Benjamin Netanyahu kuendeleza tabia yake ya kujichukulia hatua za upande mmoja, wakosoaji wake wametishia kulivunja Baraza la Mawaziri la Vita la utawala huo.
-
Afisa Mzayuni: Hatuwezi kukabiliana na mashambulizi ya Hizbullah, tunajificha tu
Feb 18, 2024 04:07Mkuu wa baraza la kitongoji cha walowezi wa Kizayuni cha Margaliot ambaye hivi karibuni aliliomba jeshi la Israel liharibu miji ya mpakani ya Lebanon, amekiri kwamba, mashambulio ya harakati ya Kiislamu ya Hizbullah ni makali mno kiasi kwamba hawawezi tena kuingia na kutoka kwa urahisi katika mji huo na kitu pekee wanachoweza kufanya ni kujificha.
-
Uhusiano wa Saudia na Syria wazidi kuimarika, Bin Salman kutembelea Damascus
Feb 18, 2024 04:06Gazeti la kimataifa la Rai Al-Youm limezungumzia kuzidi kustawi na kuimarisha uhusiano wa Riyadh na Damascus na kusema kuwa, karibuni hivi mrithi wa kiti cha ufalme wa Saudi Arabia, Mohammed bin Salman atatembelea Syria ili kuzidi kuimarisha uhusiano wa opande mbili.
-
Kiongozi wa HAMAS: Israel inabeba dhima ya kukwama mazungumzo ya kusitisha vita
Feb 17, 2024 23:30Mkuu wa Ofisi ya Kisiasa ya Harakati ya Muqawama wa Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa, utawala wa Kizayuni unawajibika kwa kushindwa kupiga hatua mazungumzo na kufikia makubaliano ya usitishaji vita katika Ukanda wa Gaza.
-
HAMAS yaiasa ICJ iibebeshe dhima Israel kwa jinai za kivita Gaza
Feb 17, 2024 08:03Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (HAMAS) imeitaka Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) iuwajibishe utawala wa Kizayuni wa Israel kutokana na jinai za kivita zinazofanywa na utawala huo pandikizi dhidi ya wananchi madhulumu wa Palestina katika Ukanda wa Gaza.