May 29, 2024 06:41 UTC
  • Bendera ya Palestina yapepea ndani ya Bunge la Ufaransa

Bendera ya Palestina imepepea katika Bunge la Ufaransa.

Kwa mujibu wa gazeti la Ufaransa Le Figaro, Sébastien Delogu, mbunge wa Ufaransa, alinyanyua na kupeperusha bendera ya Palestina kwa muda ndani ya Bunge la nchi hiyo wakati wa kipindi cha masuali kwa serikali na kwa mara nyingine tena akaonyesha uungaji mkono wake wa dhati kwa piganio tukufu la Palestina.
Hatua ya mbunge huyo wa chama cha Unyielding France katika bunge la Ufaransa imechukuliwa sambamba na ukosoaji mkubwa na wa wazi wa wanachama wa chama hicho hasa kiongozi wake mkuu Jean-Luc Melenchon na Manuel Bompard, mwanachama mwingine wa chama hicho.

Bendera ya Palestina katika Bunge la Ufaransa

Siku ya Jumanne, Jean-Luc Melenchon alionyesha sehemu ya hotuba yake aliyotoa katika mkutano wa Umoja wa Wananchi katika mji wa Besançon mashariki mwa Ufaransa na kutoa wito wa kusimamishwa mara moja utumaji silaha kwa utawala haramu wa  Israel unaofanya mauaji ya kimbari huko ukanda wa Gaza na kuitaka serikali ya Ufaransa iitambue nchi huru ya Palestina.

Wakati huohuo Manuel Bompard ameashiria shambulio la kinyama la utawala ghasibu wa Kizayuni katika kambi ya wakimbizi wa Kipalestina katika mji wa Rafah kusini mwa Ukanda wa Gaza na kusema kuwa; Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa ana hatia ya kuruhusu mashambulizi hayo.

Mbunge huyo wa Bunge la Ufaransa amesisitiza kuwa; Rais Macron ni mshirika wa jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina kwa kutotumia nyenzo zake za utendaji.

Baada ya kupita zaidi ya miezi saba, utawala haramu wa Israel huku ukiungwa mkono kikamilifu na Marekani na nchi za Magharibi umeanzisha mauaji makubwa katika Ukanda wa Gaza na Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan dhidi ya wananchi wasio na ulinzi na madhulumu wa Palestina ambayo kwa mujibu wa taarifa za hivi punde takwimu za Wizara ya Afya ya Palestina katika Ukanda wa Gaza mashambulizi hayo ya kinyama yaliyoanza tarehe 7, Oktoba 2023 yamesababisha vifo vya watu elfu 36,500 na kujeruhi zaidi ya watu elfu 81,000 huko ukanda wa Gaza.

Jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya Wapalestina zimeamsha hisia za walimwengu na katika maeneo yote ya dunia watu, serikali na taasisi mbalimbali za kimataifa zimetoa wito wa kuwaunga mkono wananchi madhulumu wa Palestina.

Waungaji mkono wa wananchi wa Palestina kote duniani wamelaani jinai za utawala ghasibu wa Kizayuni dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza kwa kufanya maandamano katika miezi ya hivi karibuni.

Waungaji mkono wananchi wa Palestina

 

Tags