Trump ataka kuchunguzwa ustahiki wa raia wa Ufaransa na Ujerumani
Donald Trump mgombea wa kiti cha urais kwa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani ametaka kuchunguzwa ustahiki wa raia wa Ufaransa na Ujerumani.
Trump amesema katika mahojiano na televisheni ya NBC kuwa kuenea ugaidi kunasababishwa na makosa yanayofanywa na nchi kama Ufaransa na Ujerumani kwa kuruhusu kupenya magaidi katika nchi hizo.
Donald Trump ameongeza kuwa iwapo atashinda katika uchaguzi wa Rais wa mwaka huu nchini Marekani, atatekeleza siasa kali kwa minajili ya kutathmini ustahiki wa watu mbalimbali.
Mgombea wa kiti cha rais kwa tiketi ya chama cha Republican nchini Marekani amedai kuwa Uingereza imejitoa ndani ya Umoja wa Ulaya kutokana na misimamo ya uchupaji mipaka huko Ulaya.
Wakati huo huo tajiri huyo wa Marekani amekosoa vikali kuteuliwa Tim Kaine kuwa Makamu wa Hillary Clinton mgombea anayetazamiwa kukiwakilisha chama cha Democratic katika uchaguzi wa Rais wa Marekani mwaka huu na kumtuhumu Seneta huyo wa jimbo la Virginia kuwa ni fisadi.