Özdemir: Saudia ndiyo chimbuko la ugaidi wa kimataifa
https://parstoday.ir/sw/news/world-i11914-Özdemir_saudia_ndiyo_chimbuko_la_ugaidi_wa_kimataifa
Mwenyekiti wa Chama cha Kijani cha Ujerumani (Green Party) amesema kuwa Saudi Arabia ndiyo chanzo cha ugaidi unaoonekana kote duniani.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jul 24, 2016 10:40 UTC
  • Özdemir: Saudia ndiyo chimbuko la ugaidi wa kimataifa

Mwenyekiti wa Chama cha Kijani cha Ujerumani (Green Party) amesema kuwa Saudi Arabia ndiyo chanzo cha ugaidi unaoonekana kote duniani.

Cem Özdemir amesema kuwa chanzo cha ugaidi duniani ni fikra za Kiwahabi za Saudi Arabia na kwamba Uwahabi unaoenezwa na Saudia ndiyo kituo kikuu cha aidiolojia za makundi yote yenye misimamo ya kufurutu ada kama Daesh, al Qaida na Boko Haram. 

Cem Özdemir amesema kuwa asilimia 90 ya mafundisho ya kidini yanayotolewa nchini Saudi Arabia yanaoana na mafundisho ya Daesh.

Mwenyekiti wa Chama cha Kijani nchini Ujerumani amezitaka nchi zote za Magharibi kutazama upya uhusiano wao na Saudi Arabia na kusema, badala ya kuitambua serikali ya Riyadh kama mshirika na kuiuzia aina mbalimbali ya silaha, zinapaswa kutambua kuwa tafsiri yenye misimamo  mikiali ya dini ya Uislamu huko Saudia ni hatari hata wa Waislamu. 

Daesh wakikata kichwa cha mateka wao

Cem Özdemir amesisitiza kuwa nchi za Magharibi zinapaswa kuona hatari hizo na zisiifumbie macho.