Oct 31, 2016 04:25 UTC
  • Wanaharakati wa haki za binadamu waandamana Ubelgiji dhidi ya Aal Saud

Wanaharakati wa kutetea haki za binadamu wameandamana mbelel ya ubalozi wa Saudi Arabia huko Brussels mji mkuu wa Ubelgiji kulalamikia na kupinga jinai za utawala wa Aal Saud.

Makumi ya wanaharakati hao wa haki za binadamu wameandamana hadi mbele ya ubalozi wa Saudia huko Brussels Ubelgiji na kulaani jinai zinazofanywa na utawala wa Aal Saudi dhidi ya raia wa Yemen, Syria na Iraq na kuzitolea wito taasisi za kimataifa kuchukua hatua za kukomesha jinai hizo. Wafanya maandamano hao walikuwa wamebeba mabango yenye picha mbalimbali zinazooonyesha jinai na mauaji yanayofanywa na utawala wa Aal Saud katika nchi za Yemen, Syria na Iraq.

Sehemu tu ya maafa yaliyosababishwa kwa raia wa Yemen kutokana na uvamizi wa kijeshi wa Saudia

Mwezi Machi mwaka jana Saudia ilianzisha uvamizi wa kijeshi wa anga dhidi ya wananchi  Yemen   kwa kuasisi muungano vamizi kwa uungaji mkono wa Marekani kwa kisingizio cha kutaka kumrejesha madarakjani rais aliyekimbia nchi Abdu Rab Mansour Hadi. Wayemen zaidi ya elfu sita wameshauliwa hadi sasa katika mashambulizi hayo ya Saudia na wengine wasiopungua milioni tatu wamekuwa wakimbizi.

Mbali na hasara, maafa na uharibifu uliosababishwa na uvamizi huo wa kijeshi huko Yemen na taasisi za miundo mbinu zikiwemo hospitali na shule zimebomolewa katika mashambulizi hayo ya Saudia na washirika wake.

Hii ni katika hali ambayo utawala wa Aal Saud unaendelea kuyaunga mkono kwa hali na mali makundi ya kigaidi huko Syria na Iraq, na hivyo kusababisha maafa na kuwafanya wahanga maelfu ya raia wa nchi mbili hizo za Kiarabu na Kiislamu.

Tags