Dec 23, 2016 07:01 UTC
  • WHO: Chanjo ya Ebola yatoa ulinzi wa asiilimia 100

Utafiti uliochapishwa katika jarida la Lancet umeonyesha kuwa chanjo ya majaribio ya ugonjwa unaosababishwa na virusi vya Ebola kwa jina la rVSV-ZEBOV inaonekana kuwa na athari kwa asilimia 100.

Imeelezwa kuwa matokeo ya utafiti huo yanatoa matumaini ya kuwezwa kuepukana na maradhi hayo yaliyosababisha vifo vya watu zaidi ya 11,000 huko magharibi mwa Afrika mwaka 2014. 

Dakta Keita Sakoba Mkurugenzi wa Idara ya Taifa ya Usalama wa Afya ya Guinea Conakry ameeleza kuwa, ugonjwa wa Ebola ulisababisha madhara makubwa nchini humo na kwamba hivi sasa wanaona fakhari kuwa wamefanikiwa kutengeneza chanjo ambayo itazuia mataifa mengine kutumbukia katika janga kama hilo lililoisibu nchi yao.

Wizara ya Afya ya Guinea Conakry ikijadili mikakati ya kupambana na maradhi ya Ebola 

Chanjo hiyo ya majaribio ilitolewa mwaka jana kwa watu waliokuwa na maingiliano na wagonjwa huko Guinea Conakry.  Miezi kadhaa baadaye baada ya majaribio yake ya mapema, Shirika la Afya Duniani lilieleza kuwa, matokeo ya awali ya chanjo hiyo ya Ebola yanatia matumaini makubwa. Majaribio ya chanjo hiyo yamejumuisha watu zaidi ya 11,000 kwa mujibu wa WHO ambayo imeongoza majaribio hayo kwa kushirikiana na Wizara ya Afya ya Guinea.

 

 

Tags