Unicef: Kuuliwa watoto wa Yemen ni jinai
Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (Unicef) limesema kuwa mshambulizi yanayofanywa na Saudi Arabia dhidi ya watoto wa Yemen ni jinai za wazi na zisizosameheka.
Grant Burchard Naibu Mkurugenzi wa Unicef nchini Yemen amesema kupitia taraifa iliyotolewa na shirika hilo kuwa watoto wa Yemen na familia zao wameathirika pakubwa na vita vya miaka miwili vya Saudia dhidi ya nchi hiyo na kwamba katika muda huo watoto wa Yemen karibu 1500 wameuawa na maelfu ya wengine wamekuwa vilema. Burchard pia amelitaja shambulizi la anga la hivi karibuni la Saudia katika marasimu ya mazishi katika mji wa Arhab Sana'a mji mkuu wa Yemen kuwa ni maafa.
Watu wanane waliuawa na wengine kumi kujeruhiwa katika shambulio la umwagaji damu lililofanywa wiki iliyopita na ndege ya kivita ya Saudi Arabia mazikoni katika eneo la Arhan kaskazini mwa mji mkuu wa Yemen Sana'a. Watoto ni miongoni mwa waliouawa katika shambulio hilo la anga la Saudia. Saudia Arabia huku ikiungwa mkono kwa hali na mali na Marekani mwezi Machi mwaka juzi ilianzisha uvamizi wa kijeshi dhidi ya wananchi wa Yemen lengo likiwa ni kumrejesha katika siasa za Yemen Rais aliyejiuzulu wa nchi hiyo Abdurabuh Mansour Hadi. Aidha watu zaidi ya elfu 38 wameuawa na kujeruhiwa kufuatia uvamizi huo wa kijeshi wa Saudia na waitifaki wake huko Yemen. Uvamizi huo wa kijeshi wa Saudia umeharibu na kubomoa miundo mbinu ya Yemen na kuwafanya mamilioni ya raia wa nchi hiyo kuwa wakimbizi khususan wanawake na watoto.