Mar 17, 2017 03:57 UTC
  • Maadui wa Waislamu washambulia msikiti mwingine nchini Marekani

Vyombo vya habari vya nchini Marekani vimeripoti habari ya kushambuliwa msikiti mwingine, kusini magharibi mwa nchi hiyo.

Televisheni ya al Alam imetangaza kuwa, watu wasiojulikana wameushambulia  msikiti wa mji wa Tuscon huko Arizona na sambamba na kuzivunjia heshima nakala za Quráni Tukufu, wamezitupa sakafuni baadhi ya nakala hizo.

Kwa upande wake, televisheni ya ABC News ya Marekani imerusha katika ukurasa wake wa Twitter picha ya mtu mmoja anayetafutwa na jeshi la polisi la jimbo la Arizona anayedhaniwa kuhusika katika uharibifu huo na kuchana nakala kadhaa za Quráni Tukufu.

Huo ni msikiti wa tano kushambuliwa nchini Marekani tangu alipoingia madarakani Rais Donald Trump mwenye chuki na wageni hasa Waislamu.

Maandamano ya wananchi wa Marekani ya kulalamikia sera mbovu za Donald Trump

 

Chuki na jinai dhidi ya Waislamu zimeongezeka mno nchini Marekani tangu alipotangazwa mshindi Donald Trump katika uchaguzi wa rais wa hivi karibuni wa Marekani uliogubikwa na matatizo mengi.

Wakati wa kampeni za uchaguzi, Trump alitumia majukwaa ya kisiasa kutoa maneno ya chuki na ya kibaguzi dhidi ya wageni na hasa Waislamu kiasi kwamba alisema, iwapo atakuwa rais wa Marekani, atapiga marufuku Waislamu kukanyaga ardhi ya Marekani. Hadi hivi sasa ameshatoa amri mara mbili ya kuzuia raia wa nchi kadhaa zenye Waislamu wengi wasiingie Marekani. 

Tags