Mar 23, 2017 03:07 UTC
  • Watano wauawa London katika hujuma ya kigaidi, makumi wajeruhiwa

Watu watano wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya mtu mmoja kushambulia watu waliokuwa wakitembea kwa miguu kwa kuwagonga kwa gari nje kidogo ya jengo la Bunge la Uingireza mjini London.

Afisa wa kikosi cha polisi ya kupambana na ugaidi ya Uingereza, Mark Rowley amesema kwa uchache polisi mmoja na wapita njia wawili ni miongoni mwa waliouawa katika shambulizi la jana kwenye Daraja la Westminster karibu na jengo la Bunge.

 Rowley ameongeza kuwa polisi watatu ni miongoni mwa waliojeruhiwa na kwamba wawili miongoni mwao wako mahututi. Amesema mtu aliyefanya shambulio hilo ameuawa kwa kupigwa risasi na makumi ya watu wengine wamejeruhiwa. 

Polisi ya Uingereza imetangaza kuwa, shambulizi hilo ni la kigaidi na kwamba uchunguzi mkubwa unafanyika kubaini uhakika wa mambo.

Miongoni mwa majeruhi wa shambulizi la Westminster, London

Vyombo vya habari vya Uingereza vimeripoti kuwa mshambuliaji huyo aliwagonga watu waliokuwa wakitembea kwa miguu kabla ya kuteremka na kumdunga kisu polisi aliyekuwa akilinda majengo ya Bunge.  

Tags