May 07, 2017 13:22 UTC
  • Waislamu na wanaharakati waandamana London, Uingereza dhidi ya Israel

Mamia ya Waislamu nchini Uingereza wamefanya maandamano katika mji mkuu London kulaani ukaliaji wa mabavu na upanuzi wa vitongoji vya walowezi za Kiyahudi katika ardhi za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu.

Waandamanaji hao wakiwemo wanaharakati wa kijamii wamelaani ukaliaji wa mabavu wa ardhi za Wapalestina kwa miongo kadhaa sasa sambamba na kuikosoa Tel Aviv kwa kuendeleza ujenzi wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina, licha ya azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa linalopinga ujenzi huo.

Waandamanaji hao wamekusanyika nje ya ubalozi wa Israel mjini London katika maadhimisho ya miaka 69 tangu utawala ghasibu wa Israel uanze kuzikalia kwa mabavu ardhi za Palestina.

Sambamba na maadhimisho hayo, Waislamu hao wa London wamefanya maandamano hayo kwa shabaha ya kuonyesha mshikamano na uungaji mkono wao kwa Wapalestina waliosusia kula katika magereza ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Gregory III Laham, Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki Quds Tukufu akishiriki maandamano dhidi ya Israel

Baadhi ya mabango yaliyokuwa yamebebwa na waandamanaji yalikuwa na maneno kama: Tunaunga mkono Muqawama dhidi ya Ugaidi wa Israel','' ''Haki kwa Wafungwa wa Kipalestina'' na ''Tunawaunga Lkono Wafungwa wa Kisiasa wa Palestina.''

Wananchi katika nchi za Morocco na Jordan wamefanya maandamano kama hayo ya London kuonyesha uungaji mkono wao kwa mamia ya mateka wa Kipalestina, ambao walianza mgomo wa chakula tangu Aprili 17.

Kadhalika shakhsia mbalimbali kama vile Waziri Mkuu wa zamani wa Lebanon na Askofu Mkuu wa Kikatoliki eneo la Quds Tukufu wametangaza kususia kula kuwaunga mkono wafungwa hao wa Kipalestina wanaoteseka katika jela na magereza ya utawala wa Kizayuni wa Israel.

Tags