China yalaani chokochoko za meli za kivita za Marekani
https://parstoday.ir/sw/news/world-i31274-china_yalaani_chokochoko_za_meli_za_kivita_za_marekani
China imelaani vikali hatua ya hivi karribuni ya meli ya kivita ya Marekani kukaribia mipaka yake ya majini katika kisiwa kimoja kinachozozaniwa katika Bahari ya China Kusini na kuitaja hatua hiyo kuwa ya kichochezi.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Jul 03, 2017 02:35 UTC
  • China yalaani chokochoko za meli za kivita za Marekani

China imelaani vikali hatua ya hivi karribuni ya meli ya kivita ya Marekani kukaribia mipaka yake ya majini katika kisiwa kimoja kinachozozaniwa katika Bahari ya China Kusini na kuitaja hatua hiyo kuwa ya kichochezi.

Vyombo vya habari vya China viliripoti Jumapili kuwa, meli ya kivita ya Marekani ijulikanayo kama USS Stethem ilifika katika Kisiwa cha Triton, ambacho ni sehemu ya Visiwa vya Paracel katika Bahari ya China Kusini. Katika kukabiliana na uchokozi huo, China ilituma meli na ndege zake za kivita kukabiliana na uchokozi huo wa Marekani.

Wizara ya Mambo ya Nje ya China imesema meli hiyo ya kivita ya Marekani  iliingia kinyume cha sheria katika maji ya nchi hiyo. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Lu Kang amesema hatua hiyo ya Marekani ni uchochezi wa kijeshi na kisiasa. Aidha ameitaka Marekani isistishe mara moja chokochoko zake hizo ambazo zinahatarisha usalama na mamlaka ya kujitawala China.

Meli ya kivita ya Marekani ikikaribia Bahari ya China Kusini

Halikadhalika ameonya kuwa, China itachukua hatua zote zinazohitajika kukabiliana na uvamizi wa Marekani.

Visiwa vya Paracel vinazozoaniwa baina ya China na nchi kadhaa jirani ingawa Beijing inasisitiza kuwa, visiwa hivyo ni milki yake. Marekani imejiingiza katika mgogoro huo na kuunga mkono nchi zinazozozoana na China.