Aug 14, 2017 15:17 UTC
  • Watu 35 wameuawa katika matukio ya ufyatuaji risasi nchini Marekani

Kituo cha takwimu za matukio ya ukatili wa utumiaji silaha moto nchini Marekani kimetangaza kuwa watu 35 wameuliwa kwenye matukio ya ufyatuaji risasi katika maeneo tofauti nchini humo.

Taarifa iliyotolewa leo na kituo hicho imeeleza kuwa watu wasiopungua 35 wameuliwa na wengine 63 wamejeruhiwa katika matukio 78 ya ufyatuaji risasi yaliyojiri kwenye kipindi cha masaa 24 yaliyopita katika majimbo mbalimbali ya Marekani.

Kwa mujibu wa ripoti ya Kituo cha takwimu za matukio ya ukatili wa utumiaji silaha moto nchini Marekani mengi ya matukio hayo ya ufyatuaji risasi yametokea katika majimbo ya Virginia, California, Pennsylvania na Illinois.

Polisi wakiwa katika eneo la mauaji

Kituo hicho cha takwimu za matukio ya ukatili wa utumiaji silaha moto kimeripoti pia kuwa matukio 184 ya ufyatuaji risasi yamesajiliwa katika muda wa masaa 48 yaliyopita ambapo watu 64 wameuliwa na wengine 133 wamejeruhiwa.

Maelfu ya watu wanauliwa na kujeruhiwa kila mwaka nchini Marekani katika matukio ya ufyatuaji risasi yanayojiri kwenye maeneo tofauti ya nchi hiyo.../

 

Tags