Bangladesh yaitaka dunia iishinikize Myanmar iacha kuwakandamiza Waislamu
https://parstoday.ir/sw/news/world-i36191-bangladesh_yaitaka_dunia_iishinikize_myanmar_iacha_kuwakandamiza_waislamu
Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuishinikiza Myanmar isitishe ukandamizaji wa Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini humo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Nov 06, 2017 02:45 UTC
  • Bangladesh yaitaka dunia iishinikize Myanmar iacha kuwakandamiza Waislamu

Waziri Mkuu wa Bangladesh Sheikh Hasina ametoa wito kwa jamii ya kimataifa kuishinikiza Myanmar isitishe ukandamizaji wa Waislamu wa jamii ya Rohingya nchini humo.

Aidha ameitaka jamii ya kimataifa isaidie kuwarejesha nyumbani wakimbizi zaidi ya laki sita Warohingya waliokimbilia Bangladesh kufuatia ukandamizaji nchini Myanmar.

Sheikh Hasina aliyasema hayo jana Jumapili katika mji mkuu wa Bangladesh, Dhaka wakati akifungua mkutano wa 63 wa kibunge wa nchi za Jumuiya ya Mdola na kuongeza kuwa, kukandamizwa Warohingya kumevuruga uthabiti katika eneo hilo.

Waislamu wa jamii ya Rohingya wakiwa katika kambi ya wakimbizi Bangladesh

Waislamu wa Rohingya wa Myanmar zaidi ya elfu sita wameshauawa na wengine zaidi ya elfu 10 kujeruhiwa hadi sasa tangu tarehe 25 mwezi Agosti mwaka huu wakati lilipoanza wimbi jipya la mashambulizi ya ukandamizaji ya jeshi la nchi hiyo dhidi ya jamii hiyo ya walio wachache katika mkoa wa Rakhine. Magenge ya Mabudha wenye misimamo mikali pia wamekuwa wakitekeleza mauaji ya umati dhidi ya Waislamu. Hadi sasa karibu Warohingya laki sita wanaripotiwa kukimbilia nchi jirani ya Bangladesh kufuatia hujuma dhidi yao katika jimbo la Rakhine nchini Myanmar.